Monday, August 10, 2015

Wanafunzi Msangamkuu sasa kutumia Kivuko bure.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio kinachofanya masafa yake kutoka Mtwara-Msangamkuu hapo jana.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwahutubia wakazi wa kata ya Msangamkuu, mkoani Mtwara mara baada ya kuzindua kivuko cha MV Mafanikio.


Jiwe la Msingi katika kivuko cha MV Mafanikio kilichozinduliwa na Ras Kikwete jana mkoani Mtwara.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akielekea katika uwanja maalum katika kata ya Msangamkuu kwa ajili ya kuwahutubia wakaazi wa kata hiyo jana


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili katika eneo la wazi Msangamkuu ambako aliandaliwa kwa ajili ya kutoa hotuba yake kwa wakaazi wa kata hiyo.




Na Juma Mohamed, Mtwara.
 
WANAFUNZI wakaazi wa Kata ya Msangamkuu wanaosoma mjini Mtwara wamenufaika na ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. John P. Magufuli aliyetoa tamko la kuto tozwa nauli wanafunzi wa ngazi zote watakao vuka kivuko cha Mtwara-Msangamkuu MV Mafanikio. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, akizungumza na wakaazi wa kata ya Msangamkuu.

 Rais Kikwete, amezindua kivuko hicho jana kinachosafirisha abiria kutoka Mtwara-Msangamkuu, chenye uwezo wa kubeba abiria 100 na magari sita kwa wakati mmoja.
Akiwahutubia wakazi wa kata ya Msangamkuu, Rais Kikwete amewaahidi wananchi wa kata hiyo kuwakamilishia mradi wa maji ambao unatekelezwa huku ukikabiliwa na uhaba wa fedha kiasi cha shilingi milioni 400.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais, waziri wa ujenzi na mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. John Magufuli, ameagiza wanafunzi wa ngazi zote kusafiri bure kwa kutumia kivuko hicho ambacho ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na wakaazi wa kata ya Msangamkuu jana.

Aidha, alisema watu wazima wataendelea kuchangia kwa kiasi kidogo ambacho kinaendelea kutumika cha sh. 300 ambacho kilipangwa na wahusika.

No comments: