RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi ujao
anatarajia kuzindua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo kata ya
Mtanda, mjini Lindi.
Rais Kikwete
atawasili eneo hili akitokea Wilayani Kilwa ambako alikuwa na hafla ya kuzindua
barabara ya kilomita 60 ya Somanga, ambapo ameongozana na viongozi wengine wa
serikali ikiwa ni pamoja na mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dk. John Pombe Magufuli.
Kwamujibu wa
taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando, jumla ya nyumba 30 ambazo
Mhe. Rais atazindua umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.004 mpaka
kukamilika kwake.
No comments:
Post a Comment