Sunday, October 14, 2012

WANACHUO WALIPA KISASI NIGERIA, BAADA YA KUGUNDUA KUWA WALIYOUWAWA HAWAKUWA NA HATIA

 

.
Ni taarifa ya kuhuzunisha kuhusu wanachuo wanne wa Nigeria waliouwawa na wananchi wenye hasira na waliojichukulia sheria mikononi kwenye kijiji cha Aluu baada ya wanachuo hao kutuhumiwa kuwa wezi na mtu ambae mmoja wao alikua anamdai pesa.
Baada ya vifo vyao ukweli ndio umejulikana kwamba wanachuo hao hawakuwa wezi bali walisingiziwa, kutokana na hilo wanachuo wenzao wenye hasira waliingia mtaani kwenye kijiji cha Aluu ili kulipa kisasi.
Huyu mzee wa miaka 65 anasema katika miaka yake yote ya kazi ndio aliweza kujipatia hizi mali ambazo ndio zimeharibiwa na wanachuo waliolipa kisasi, hajui ataipeleka wapi familia yake ya watoto 15.
Wamechoma moto nyumba kadhaa, wamechukua mali za watu wakiwemo wafanyabiashara pamoja na pesa zao na kufanya uharibifu mwingine na fujo juu ikiwa ni kulipa kisasi kwa wananchi wa kijiji hicho ambacho hivi karibuni kimekua kikikumbwa na matukio ya uhalifu ndio maana ilikua rahisi kuamini pia vijana hao wanne walikua wezi ambapo wakazi wa kijiji cha Aluu walihama makazi yao kwa kukimbia baada ya kusikia kundi la wanachuo hao likija kwa nguvu.
Hawa ndio wanafunzi wanne waliouwawa kinyama, walivuliwa nguo na kutembezwa uchi kabla ya kuchomwa moto hadharani.
.
 
SOURCE:MILLAD AYO

No comments: