Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza rasmi Oktoba 24
mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa tofauti
katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mechi
za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni
Burkina Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small
Kids (Majimaji, Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja
wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa).
Mkamba
Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo
Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi
za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa
Polisi Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids
(Majimaji, Songea), Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro)
na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT (Wambi, Mufindi).
Raundi
ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale
JKT (Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela,
Sumbawanga), Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi
Iringa vs Kurugenzi Mufindi (Samora, Iringa).
Kundi
B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati
Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na
Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Raundi
ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs Green Warriors
(Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini, Pwani)
wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini,
Pwani) na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam
(Chamazi, Dar es Salaam).
Novemba
1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United (Mabatini, Pwani),
Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar
es Salaam), Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es
Salaam) na Transit Camp vs Moro United (Mabatini, Pwani).
Kundi
C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake Tanganyika,
Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara
(Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
Raundi
ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma (Ali
Hassan Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga),
Kanembwa FC vs Morani (Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino
Rangers (Kirumba, Mwanza).
Oktoba
31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers (Karume,
Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi Dodoma vs
Pamba (Jamhuri, Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake Tanganyika,
Kigoma).
No comments:
Post a Comment