TFF YAOMBOLEZA MSIBA WA MELI
Z’BAR
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya meli ya Mv Skagit
iliyotokea jana (Julai 18 mwaka huu) na kupoteza maisha ya karibu abiria 100
waliokuwemo kwenye chombo hicho.
Ajali hiyo mbaya iliyotokea
karibu na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar na kusababisha vifo vya watu wengi ni
msiba mkubwa, si kwa wadau wa mpira wa miguu pekee, bali kwa wananchi wote wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo tunatoa pole na salamu
za rambirambi kwa ndugu wa marehemu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na
wote walioathirika na kuguswa na msiba huo mkubwa.
Kutokana na msiba huo, mechi
mbili za leo kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame)
kati ya Atletico ya Burundi na El Salam Wau ya Sudan Kusini na ile ya Mafunzo ya
Zanzibar dhidi ya Tusker ya Kenya zitachezwa huku wachezaji wa timu zote wakivaa
vitambaa vyeusi.
Mbali ya vitambaa hivyo, pia
kutakuwa na dakika moja ya kukaa kimya kwa ajili ya kuomboleza vifo hivyo kabla
ya kuanza mechi hizo zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi ya
kwanza itaanza saa 8.00 mchana wakati ya pili itachezwa kuanzia saa 10.00 jioni.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment