Jamaa mmoja mida hii chupuchupu agombewe na
wanachama wa Yanga, baada ya kufika makao makuu ya klabu, Jangwani akiwa na
barua ya wakili ya kushauri uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Jumapili
uahirishwe. Kilichomponza ni kwamba, alipofika mlango wa kuingia klabuni,
akasema anataka kumuona Katibu Mkuu, ana barua ya Mahakama ya kuzuia uchaguzi.
Watu kusikia hivyo wakamvaa, kwanza wakampora begi lake wakachukua barua
wakaisoma. Wakagundua ni ya wakili tu na haina nguvu, ndipo wakamrudishia barua
yake na kumfukuza, tena wakimuonya asionekane kabisa katika viunga hivyo. Soma
barua yenyewe….
YANGA FANS FACEBOOK WAMWAGA MAJI KLABUNI
Beki wa Yanga, Ladislaus Mbogo kulia, akipokea msaasa huo |
Mwesigwa alikuwa anaendelea na mambo yake |
Na Princess
Asia
Wanachama na mashabiki wa
Yanga wa kundi cha Young Africans SC Fans katika facebook, leo wamekabidhi
msaada wa maji ya kunywa kwa ajili ya wachezaji wa klabu hiyo, wenye thamani ya
Sh. 80,000 ofisini kwa Katibu Mkuu wa Yanga, makutano ya mitaa ya Twiga na
Jangwani, Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo,
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Innocent Mwingira alisema kwamba wameamua kutoa
msaada huo ili pamoja na kudhihirisha mapenzi yao kwa klabu yao, lakini pia
kufungua milango kwa watu wengine wenye uwezo wa kutoa misaada midogomidogo ya
aina hiyo, wajitokeze.
“Tunaamini tulichotoa
kitasaidia klabu, japo kwa siku mbili, Yanga ina mamilioni ya wapenzi, kama
wakijitokeza wengine na wengine, tuna hakika klabu yetu haitakuwa na matatizo
madogo madogo, hivyo sisi tunawaomba na wengine pia waige mfano
huu,”alisema.
Akipokea msaada huo, beki wa
Yanga Ladislaus Mbogo alisema kwamba kwa niaba ya wachezaji wenzake anashukuru
kwa msaada huo kwani hiyo ni ishara kwamba wapenzi hao wapo nyuma ya
wachezaji.
Katibu wa Yanga, Selestine Mwesigwa aliwashukuru wapenzi hao na kusema huo ni mfano wa kuigwa na akafungua milango kwa wapenzi wengine wowote wa Yanga, kujitokeza wakati wowote kutoa chochote walichonacho.
Katibu wa Yanga, Selestine Mwesigwa aliwashukuru wapenzi hao na kusema huo ni mfano wa kuigwa na akafungua milango kwa wapenzi wengine wowote wa Yanga, kujitokeza wakati wowote kutoa chochote walichonacho.
Kwa
upande wake, Katibu Msaidizi wa kikundi hicho, Fadhila Lemba alisema kwamba
msaada huo kwao ni mwanzo tu na watakuwa wakijikusanya na kutoa zaidi.
MWANZA YATINGA FAINALI COPA COCA COLA
Na Princess
Asia
MWANZA imejipatia tiketi ya
kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Julai
13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi dakika 90 za kawaida
zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza walitangulia kufunga
dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti
dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.
Mabao mengine ya Mwanza
yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili) yalifunga katika
dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson
Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.
Nusu fainali ya pili itachezwa
leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo fainali iliibamiza
Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Dodoma.
NYIGU WATOTO WAJA KUIVAA NGORONGORO
Frank
Damayo, mmoja wa nyota wa Ngorongoro |
Na Prince
Akbar
TIMU ya taifa ya Rwanda ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 inatarajia kuwasili Dar es Salaam leo mchana
(Julai 13 mwaka huu) kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki
dhidi ya Ngorongoro Heroes.
Rwanda yenye msafara wa watu
27 wakiwemo wachezaji 20 itafikia hoteli ya Sapphire. Mechi hizo zitachezwa
Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi na Julai 16 mwaka huu Uwanja wa
Taifa.
Ngorongoro Heroes tayari iko
kambini chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Adolf Rishard kujiwinda
kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya maandalizi ya kuivaa
Nigeria.
Mechi dhidi ya Nigeria ambayo
ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika
zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TUSKER WATUA LEO KUKAMILISHA IDADI TIMU ZA KAGAME 2012
Kikosin cha Tusker FC |
Na Prince
Akbar
MABINGWA wa zamani Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Tusker ya Kenya na Ports ya
Djibouti zinawasili leo jioni kukamilisha idadi ya timu 11 zinazoshiriki
mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mechi za kesho ni APR ya
Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na
kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico
ya Burundi.
Timu zote kutoka nje ya
mazoezi zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo zitavitumia kwa mujibu wa
ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makazi
ya timu hizo na viwanja vya mazoezi ni kama ifuatavyo;
Timu: Uwanja
wa mazoezi: Accommodation:
APR
(Rwanda) Mabibo Hostel - Marriott Hotel (Mabibo
External)
AS
Vita (Congo) University of Dar es Salaam - Chichi Hotel
(Kinondoni)
Atletico (Burundi) Mabibo
Hostel - Lunch Time Hotel (Mabibo
Hostel)
Azam (Tanzania) Azam
Complex - Azam Complex (Chamazi)
El
Salam Wau (S. Sudan) Zanaki Sekondari - Rungwe Hotel
(Kariakoo)
Mafunzo (Z’bar)
Kinesi - Rombo Green View Hotel
(Sinza)
Ports (Djibouti)
Kinesi - Rombo Green View Hotel
(Sinza)
Simba (Tanzania)
……………………. – Vina Hotel (Mabibo
Makutano)
Tusker (Kenya) Zanaki
Sekondari - Rungwe Hotel (Kariakoo)
URA
(Uganda) Loyola - Valentino Royal
Hotel (Kariakoo)
Yanga (Tanzania)
…………………. – ……………………….
SAFU YA UONGOZI YANGA HII HAPA, KASWAHILI AIPIGA ZENGWE
Safu ya uongozi iliyokemewa na Kaswahili, lakini si inafaa kabisa hii jamani? |
No comments:
Post a Comment