Friday, July 6, 2012

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA VAN PERSIE NA WENZIE

Kwa mara ya pili kwenye maisha yake ya soka - kocha mkongwe Luis Van Gaal hatimaye amepata nafasi ya kusahihisha makosa yake aliyoyafanya miaka sita iliyopita kwa kuiongoza Uholanzi kukosa nafasi ya kucheza kwenye kombe ladunia kwa mara ya kwanza.

Siku kadhaa baada ya kocha Bert van Marwijk kujiuzulu kuifundisha Uholanzi baada ya kucheza kwa kiwango kibovu kwenye Euro 2012, leo hii amepata mrithi wake - Luis van Gaal.

Van Gaal kocha wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich anamrithi Bert, huku ikiwa ni kipindi chake cha pili kuiongoza Holland.

Baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari Van Gaal alisema: "Ni changamoto niliyokuwa nikiisubiri sana, nashukuru nina nafasi ya kurekebisha palipoenda vibaya mara mwisho nilivyokuwa mwalaimu wa timu ya taifa."

Kocha huyu mwenye miaka 60 amesaini mkataba wa ambao utampeleka mpaka kwenye fainali za kombe la dunia 2014.
 

MCHAKATO WA LIGI KUENDESHWA KAMPUNI WAFIKIA ASILIMIA 95 SASA

Hatimaye mchakato wa vilabu kuweza kufungua kampuni itakayosimamia umeanza kufikia mwishoni.

Kwa taarifa nilizonazo leo kumekuwepo na kikao cha mwisho kilichokaa kwa kuwahusisha viongozi kutoka kwenye vilabu vyote vya ligi kuu ambao ndio wanaounda kampuni itayosimamia ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.


Kwenye kikao hicho mambo yote muhimu katika kuelekea kwenye mchakato huo wa kuanzishwa kwa kampuni na sasa kilichobakia ifikapo wiki ijayo - viongozi hao wa vilabu watapeleka mfumo mzima na utaratibu waliopanga kwa namna ya kuendeshwa kwa ligi msimu kwa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka kwa ajili ya kupata mawazo tofauti ili kuleta maboresho kama yatakuwepo - na mchakato wa kuifungua kampuni kuanza mara moja

No comments: