LULU AENDELEA KUSOTA SEGEREA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana iliahirisha tena kesi ya mauaji ya msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba, inayomkabili Elizabeth Michael ‘Lulu’ hadi Juni 4, kwa maelezo kuwa jalada la kesi hiyo limeitwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Lulu kupitia mawakili wake Kenned Fungamtama, Peter Kibatara, Fulgence Masawe na Joaquine De- Melon, Mei 15 mwaka huu, aliwasilisha ombi Na.46/2012 chini ya hati ya dharura iliyokithiri Mahakama Kuu, akiomba iamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulishughulikia ombi lake la kutaka kesi hiyo isikilizwe katika Mahakama ya Watoto kwa sababu ana umri chini ya miaka 18.
Mei 18 mwaka huu, uongozi wa Mahakama Kuu ukampangia Jaji Dk. Fauz Twaibu kusikiliza ombi hilo , ambalo atalisikiliza Mei 28 mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa ombi hilo, Lulu ambaye pia ni msanii wa filamu, anadai kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando Mei 7 mwaka huu, alikataa kutoa uamuzi wa kutaka kesi hiyo ihamishiwe katika mahakama ya watoto na badala yake akasema mahakama hiyo haina mamlaka na kuwashauri mawakili wake kuwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu.
Wakili Fungamtama alidai katika hati hiyo ya madai kuwa, Hakimu Mmbando alijielekeza vibaya kwa kusema kuwa mahakama ile ilikuwa haina mamlaka ya kusikiliza ombi lao, kwa hiyo wanaiomba Mahakama Kuu imwelekeze hakimu huyo asilikize ombi lao na alitolee maamuzi na kuwa endapo itabaini vinginevyo basi mahakama hiyo ya juu itoe tafsiri ya umri kuhusu ombi hilo .
Lulu alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu akitajwa kuwa mshukiwa namba moja katika kesi ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican , Sinza jijini Dar es Salaam .
Monday, May 21, 2012
RIHANNA AWATOROKA JAY Z, KANYE NA KUJIWEKA KWA DROGBA
Published: Today at 00:59
JOHN TERRY si pekee aliyesherehekea taji la ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya la Chelsea – Rihanna pia.
Mwimbaji huyo wa Bajan aliungana na wachezaji wa Blues katika pati la ubingwa usiku.
Aliwasili klabu la West End, Boujis baada ya kuachana na Jay-Z na Kanye West usiku huo wakiwa kwenye tamasha.
Alikimbilia kwenye pati la wachezaji na alipofika tu akamvaa Didier Drogba — ambaye penalti ya mwisho iliimaliza Bayern Munich nchini Ujerumani Jumamosi. Chanzo kilisema: “Rihanna alimfuata Didier, Jose Bosingwa, Salomon Kalou, Michael Essien na Raul Meireles na wakatengenza mduara kwenye meza yao.
“Wachezaji walifurahia kukutana naye, lakini alikuwa karibu zaidi na Didier na alikuwa akicheza naye.”
Baadaye aka- tweet picha aliyopiga na mshambuliaji huyoa akiiandikia: “THEE DIDIER DROGBA #thereisaGod.” Lakini hakuwa mwanamke pekee aliyefurahia pati la Chelsea.
Christine Bleakley aliungana na mpenzi wake Frank Lampard, John Obi Mikel na Carlton Cole katika klabu ya Mayfair, Aura.
WACHEZAJI ENGLAND WAPEWA HADI CHUPI VIFAA VYA EURO 2012
Published: Today at 01:11
WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya England, watakwenda kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 bila chupi.
Hiyo ni kwa sababu Chama cha Soka England (FA) kitawapa wachezaji wote wa Roy Hodgson vifaa vyote ikiwemo chupi za timu.
Kipa namba moja wa Norwich, John Ruddy, aliyeongea na Hodgson, alisema: “Nimeambiwa na nichukue viatu, glavu, vifaa vya mazoezi, na nguo chache za kawaida na karatasi (za choo). Ninafurahi kila kitu kitakuwa kimeandaliwa kwa ajili yangu huko.
“Tumepata suti na wanaandaa chupi kwa ajili yetu. Ni kweli, lakini hiyo ndio faida ya kuwa katika kikosi cha England.
Nguo hizo zitasambazwa na kampuni ya M&S, wakati England itaweka kambi yake katika hoteli ya katikati ya jiji, Krakow, Poland.
Hapo ni jirani na kambi ya jeshi la Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Nazi, Auschwitz na FA imempanga kutembelea na wachezaji.
DROGBA AANGUA KILIO, MACHOZI DEBE AKIWAAGA WACHEZAJI WENZAKE CHESLEA
Published: 21st May 2012
DIDIER DROGBA alibubujikwa na machozi wakati akiwaambia wachezaji wenzake: ‘Naondoka.’
Mshambuliaji huyo hatari amesema inamuuma moyoni kufikia tamati ya miaka minane ya kuwa na Chelsea.
Drogba alizungumza huku analia wakati anawaambia John Terry, Frank Lampard na wengineo: ‘Hatutakuwa pamoja tena msimu ujao.’
Alitoa tamko hilo la kushitua katika sherehe za ubingwa wa Blues, saa 24 baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kuungana na mchezaji mwenzake aliyekuwa naye Chelsea, Nicolas Anelka katika klabu ya Shanghai ya China kwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
Lakini uhamisho huo umeingia shaka jana usiku, baada ya kuibuka habari, kocha Anelka amekwaruzana na wamiliki wa klabu hiyo ya Shanghai.
Drogba alisema: “Ingawa ni miaka mitatu sasa tangu niseme nataka kuondoka, inaniwia vigumu kukubali nimefikia mwisho na klabu hii — hususan tangu nikatae mwisho huu.”
Drogba aliliambia jarida la Ufaransa: “Nisingeweza kujiona nimekaa benchi nawaangalia wachezaji wengine wanacheza, wakati klabu inapanga kujenga timu mpya.
Anelka amesaidia mawasiliano kati ya Shanghai na Drogba kufikia sehemu n zuri.
Lakini Mfaransa huyo, hafurahishwi na hali ya mambo anayokabiliana huko tangu avue dakluga zake na kukaa kwenye benchi la ufundi, akirithi mikoba ya Jean Tigana mwezi uliopita na anaweza kuamua kuondoka.
CHELSEA WAMUAMBIA TORRES; WEWE WA HAPA HAPA TU
JUVENTUS KUMNG'OA DZEKO MAN CITY
KLABU ya Juventus itahamishia mawindo yake kwa mshambuliaji Manchester City, Edin Dzeko mwenye umri wa miaka 26, wakati wakijiandaa kujitoa kwenye mbio za kuwania saini ya mshasmbuliaji wa Arsenal, Robin van Persie mwenye umri wa miaka 28.
MANCHESTER City inajipanga vema kutumia mwanya wa Juve kujitoa kwenye mbio za kumuwania Van Persie, wakati Kibibi Kizee hicho cha Turin inaelezwa kinaweza kuhamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez mwenye umri wa miaka 25 sambamba na Dzeko.
KLABU ya Tottenham inamtaka mshambuliaji mwenye umri wa miaka 25-wa Marseille, Loic Remy na inaweza kubadilishana mchezaji wake Luka Modric mwenye umri wa miaka 26, kwa mchezaji wa Real Madrid, Lassana Diarra mwenye umri wa miaka 27.
QPR inatarajiwa kufanya usajili wa nguvu kwa kumchukua kipa mkongwe wa Aston Villa, Shay Given mwenye umri wa miaka 36, ambaye alicheza chini ya kocha wa Rangers, Mark Hughes katika klabu ya Manchester City. Mchezaji mwenye umri wa miaka 31 wa West Ham, Robert Green naye anaweza kuingia rada hizo.
KLABU iliyorejea Ligi Kuu ya England, West Ham, wameingiwa na hofu ya kumpoteza nyota wao Robert Green kutokana na kudai mshahara mkubwa.
KOCHA wa QPR, Hughes pia anaweza kuhamishia ndoana zake kwa mshambuliaji wa Wigan, Victor Moses mwenye umri wa miaka 21.
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich ametoa ruhusa klabu kusajili mchezaji yeyote bila kujali gharama, akiwemo nyota wa Lille, Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 21, mshambuliaji wa Porto, Hulk mwenye umri wa miaka 25, na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Falcao mwenye umri wa miaka 26.
KLABU ya Barcelona inajiandaa kutoa ofa ya pauni Milioni 10 kumnasa beki Muargentina wa Manchester City, Pablo Zabaleta, mwenye umri wa miaka 27.
KLABU ya Chelsea imeipa Arsenal hadi wiki ijayo kutoa jibu kama inataka kumsajili moja kwa moja kiungo wanayemtupia kwa mkopo hivi sasa, Myahudi Yossi Benayoun mwenye umri wa miaka 32.
MWENYEKITI wa Tottenham, Daniel Levy amesafiri hadi Uholanzi jana kufanya mpango wa kumsajili beki Mbelgiji wa Ajax, Jan Vertonghen mwenye umri wa miaka 25, ambaye pia anatakiwa na klabu za Arsenal na AC Milan.
KLABU ya Blackpool ya Daraja la Kwanza England, inataka kumchukua moja kwa moja mshambuliaji mwenye umri wa miaka 29 wa Swansea, Stephen Dobbie wanayemtumia kwa mkopo hivi sasa.
MARTINEZ KATIKA KIKAO KINGINE NA WAMILIKI WA LIVERPOOL MAREKANI
KOCHA Roberto Martinez anajiandaa kukutana na wamiliki wa klabu ya Liverpool Marekani kesho, baada ya kufanya nao mazungumzo ya awali England mwishoni mwa wiki.
KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello anaimezea mate nafasi hya kazi iliyo wazi Uwanja wa Anfield, lakini hana mawasiliano na Liverpool.
KLABU ya Chelsea imejifanya kama haijasikia lolote kutoka kwa mshambuliaji wake Fernando Torres aliyelalamikia maisha yake asiyoyafurahia Stamford Bridge, lakini imemuambia Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka 28, kwamba haendi popote.
MMILIKI wa Chelsea,Roman Abramovich binafsi amemuhakikishia maisha bora Torres katika mustakabali wake Chelsea.
Randy Lerner atasafiri hadi England kesho, wakati Aston Villa ikikaribia kumalizana na kocha mpya. Kocha wa Molde, Ole Gunnar Solskjaer ndiye anapewa nafasi hiyo lakini Kocha wa Norway, Paul Lambert na kocha wa Brighton, Gus Poyet pia nao wanapewa nafasi.
KIUNGO Joe Cole anafikiri anaweza kuwa na mafanikio Liverpool, lakini tu iwapo atacheza dimba la kubwa.
BALOTELLI AKOROFISHANA NA NYWELE ZAKE SASA
BAADA ya kuambia aepuke matatizo na kocha wa Italia, Cesare Prandelli, mshambuliaji chipukizi Mario Balotelli amekuwa akijaribu mitindo mbalimbali ya mikato ya nywele, ukiwemo wa Carlos Valderrama
No comments:
Post a Comment