Tuesday, May 22, 2012

DOX COSMETICS & BOUTIQUE MAHALI SAHIHI PAKUJIPATIA BIDHAA ZA KISASA

v iatuz kwa Wadada na Kinamama.
Weaving Original kwa kinadada.



Hand bags za ukweli.
Original Perfumes za Designers wakubwa duniani.
Original Perfumes za Designers wakubwa duniani.



WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), wamempa kura za kishindo Antony Mtaka kuwa Rais wa Shirikisho hilo akimbwaga Kanali mstaafu, Juma Ikangaa.
Katika nafasi hiyo, Mtaka ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomelo, Morogoro, alishinda kwa kura 50 dhidi ya 29 za Ikangaa, Katibu Mkuu wa zamani wa shirikisho hilo wakati huo ikijulikama kama TAAA.
Mtaka alipata kura hizo katika kura za marudio baada ya raundi ya kwanza kukosekana mshindi wa moja kwa moja miongoni mwa wagombea wanne waliokuwa wamejitosa katika nafasi hiyo kwa Ikangaa kupata kura 25 na Mtaka kura 36.
Waliochemkia raundi ya kwanza ni Francis John aliyeambulia kura 15 na Henry Nyiti aliyepata kura 7,hivyo raundi ya pili kushudia ushindani mkali kati ya Ikangaa na Mtaka.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo majira ya saa 3:30 usiku, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo, Henry Tandau, alisema kurudiwa kwa nafasi ya Rais na Katibu Mkuu, ilitokana na wagombea kushindwa kufikia asilimia iliyohitajika kwa mujibu wa kanuni.
Ushindani mwingine ulikuwa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu iliyokuwa ikishindaniwa na watu wanne, akiwemo Suleiman Nyambui aliyekuwa akitetea, John Bayo, Zainab Mbiro na John Manyama, lakini Nyambui alishinda kwa kura 41 dhidi ya 38 za Bayo, katika raundi ya pili.
Wagombea wawili katika nafasi tofauti, Makamu wa Kwanza wa Rais (Utawala) ilikwenda kwa William Kallaghe, aliyekuwa mgombea pekee kwa kura 78.
Katika nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais (Ufundi), iliyokuwa ikiwaniwa na wagombea wawili, Dk. Hamad Ndee alishinda kwa kura 55, akimbwaga Herman Ndisa aliyepata kura 42.
Nafasi nyingine iliyokuwa na ushindani ni Katibu Mkuu Msaidizi , iliyokuwa ikiwaniwa na watu wanne, lakini Ombeni Zavalla akishinda kwa kura 40, Julius Murunya (32), Lucas Nkungu na Leonard Mandara, kila mmoja akipata tatu.
Nafasi ya Mweka Hazina ilikuwa na mgombea mmoja, Is- Haq Seleman, aliyepata ushindi wa kimbunga wa kura 78kati ya 79.
Mbali ya nafasi ya Rais na Katibu Mkuu, kivumbi kingine kilikuwa kwenye nafasi 10 za ujumbe wa shirikisho hilo, zilizokuwa zikiwaniwa na wanachama zaidi ya 30.
Hata hivyo, mhariri wa michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo, alifunga pazia la nafasi zilizokuwa zikiwania baada ya kupata kura 37, akiungana na Mwinga Mwanjala ( 53), Lwiza John (50), Peter Mwita ( 50), Zakaria Gwandu ( 47)., Meta Petro Bare ( 46), Zakaria Barie (45), Rehama Killo( 42), Robert Kalyahe ( 41) na Christian Matembo (38).


Bi. Fatma Kange akiongea na wadau wa Sanaa kuhusu mfumo maalum wa kimataifa wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbali wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA Godfrey Lebejo na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA wiki hii. Alieleza kuwa, ni wakati sasa wa kuirasimisha sekta ya Sanaa.
Mtendaji kutoka Kampuni ya Global Standard One (GS1), Andrew Karumuna akionesha moja ya kazi ya Msanii Judith Wambura (Lady Jay Dee) iliyowekewa alama maalum ya kimataifa ya utambuzi na udhibiti wa bidhaa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Lady Jay Dee ni msanii pekee ambaye amekwishaingia na kuanza kunufaika na mfumo huu.

Mdau na mkereketwa wa Sanaa na Jukwaa la Sanaa, Francis Kaswahili akiuliza na kuchangia mada kuhusu mfumo huo wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za Sanaa.
Mdau huyu alipongeza ujio wa mfumo huu lakini akataka Wasanii wahamasishwe kuingia katika mfumo ili kudhibiti uharamia.
Sehemu ya Wadau wa Jukwaa la sanaa
Na Mwandishi Wetu
Huenda kilio cha wasanii juu ya wizi wa kazi zao kikapungua kama si kufikia kikomo iwapo wasanii wataamka na kushirikiana na kampuni ya Global Standard One (GS1) ambayo imekuja na mfumo wa kimataifa wa kutambua na kudhibiti kazi za Sanaa.
Akizungumza wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Fatma Kange alisema kuwa, mfumo huo wa kuziwekea alama ya utambuzi ya kimataifa (barcode) kazi za wasanii utasaidia kudhibiti uharamia kwenye sekta ya sanaa na kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi.
“Mfumo huu ni wa kimataifa, umekuwa ukitumika duniani kote miaka 38 iliyopita, hapa kwetu ni mpya kabisa. Ni mfumo wa kutambua bidhaa halali kwa kuziwekea alama maalum (barcode) ambayo itazifanya zitambuliwe kimataifa na kutokughushiwa” alisema Bi. Kange.
Aliongeza kuwa, mfumo huo unalenga kurasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwafanya wasanii kwanza kujisajili na baadaye kazi zao kuwekewa alama maalum ambapo sasa watajua idadi halisi ya nakala (bidhaa za sanaa) walizozalisha, fedha walizoingiza na zaidi kutazuia kazi zao kuuzwa hovyo mitaani pasipokufuata taratibu.
“Lengo ni kazi za wasanii kutambuliwa kimataifa, kuuzwa kwenye maduka makubwa na kupewa thamani halisi. Wenzetu katika nchi zilizoendelea wako mbali katika hili, kazi zao zinauzwa kwenye art stores tu (maduka maalum ya kazi za Sanaa)” alisisitiza Kange.
Akieleza jinsi Wasanii watakavyojiunga, Bi. Kange alisema kuwa, wako kwenye mikakati ya kuwaelimisha Wasanii lakini akasisitiza kuwa, mfumo huo huendeshwa kwa wasanii wenyewe kuridhia na baadaye kazi zao kuwekewa alama hiyo ambapo hukatwa kiwango kidogo sana cha fedha baada ya kukubaliana na wasanii wote.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema kuwa, kwa muda mrefu sekta ya Sanaa imekuwa ikichukuliwa kama ya burudani tu kwa hiyo muda umefika wa watanzania kuichukulia Sanaa kama biashara na kuipa thamani halisi.
“Kwa sasa Sanaa imekubalika, ule wakati wa kuiona kama burudani tu umepita. Hatuna ujanja lazima tuirasimishe sekta ya Sanaa” alisisitiza.
Aliwaahidi Wasanii kupitia mashirikisho na vyama vyao kuwa, kutakuwa na vikao vya mara kwa mara na kampuni hii ili kuona ni kwa kiwango gani suala la udhibiti na utambuzi wa kazi zao kupitia nembo hii linaweza kutekelezwa.

Monday, May 21, 2012

SIMBA YAMTIA PINGU MILOVAN

Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kulia, Milovan katikati na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Ibrahim Masoud walipokuwa wakisaini mkataba wa kwanza na Mserbia huyo mwaka jana.
KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake Mserbia, Profesa Milovan Cirkovic baada ya kuridhishwa na kazi yake kwa kipindi cha nusu msimu alichokuwa na timu hiyo tangu arithi mikoba ya Mganda, Moses Basena.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema jioni hii kwamba Milovan atakuwa kocha wa Simba kwa miaka miwili zaidi tangu sasa baada ya kuongezewa mkataba.
“Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho sisi kama viongozi tumekishuhudia Simba chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni kwa nini tusimuongeze mkataba,”alisema Kaburu.
Pamoja na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara kwa kishindo, Milovan aliiwezesha Simba kufika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan, baada ya sare ya jumla ya 3-3

No comments: