MTWARA
Baadhi ya wagonjwa
katika kituo cha afya cha Likombe, manispaa ya Mtwara Mikindani wameipongeza
serikali kwa kupanua wigo wa huduma za matibabu kupitia kadi za Mfuo wa Afya ya
Jamii CHF, kutoka ngazi ya halmashauri mpaka kufikia ngazi za mikoa kupitia mpango
mpya wa CHF ILIYOBORESHWA.
Wakizungumza kituoni
hapo, wamesema awali huduma hizo zilikua zinatolewa kupitia Zahanati, vituo vya
afya na hospitali za wilaya husika jambo ambalo lilikua ni changamoto endapo
mwananchi atahitaji matibabu akiwa nje ya wilaya yake.
“Kutokana na
uboreshaji ambao sasaivi tunategemea unakuja huko mbele, tunafarijika kuona
serikali kwa kushirikiana na wizara ya afya wameweza kuona hivyo watu waweze ku
‘Cover’ eneo kubwa la matibabu.” Alisema Iddi Saidi, mkazi wa Mtwara.
Dokta Nuru Nankuna, ni
mganga mfawidhi wa kituo cha afya Likombe, akaeleza mapokeo ya mpango huo na
utakavyosaidia kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma, huku Mratibu wa mpango wa
malipo kwa ufanisi kutoka wizara ya TAMISEMI, Dokta Athumani Pembe akieleza
uwamuzi wa serikali kupeleka fedha za afya moja kwa moja vituoni.
Mratibu wa Mpago wa Malipo kwa Utumishi RBF kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dokta Athumani Pembe, akitoa somo kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara. Mikoa yenye wawakilishi katika mafunzo hayo ya siku Tano ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es Salaam
Ofisi ya Rais TAMISEMI
imeshirikiana na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, kuwezesha
vituo vya kutolea huduma za afya kupokea fedha za Health Basket Fund (HBF) moja
kwa moja kwenye akaunti zao.
|
Baadhi ya watendaji wa sekta ya afya wakiwa katika makundi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya elimu wanayopatiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo yanayotolewa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 kwa ufadhili wa shirika la USAID. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara na kushirikisha watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dar es Salaam na Pwani.
|
|
Maofisa wa mradi wa PS3 wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya yanayotolewa na Mradi huo kwa ufadhili wa shirika la USAID. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara na kushirikisha watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dar es Salaam na Pwani.
|
|
Kiongozi wa mifumo ya fedha Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, Dokta Gemini Mtei akijadili jambo na mratibu wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi kutoka TAMISEMI, katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya afya. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara na kushirikisha watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dar es Salaam na Pwani.
|
|
Baadhi ya watendaji wa sekta ya afya wakiwa katika makundi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya elimu wanayopatiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo yanayotolewa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 kwa ufadhili wa shirika la USAID. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara na kushirikisha watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dar es Salaam na Pwani.
|
|
Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 mkoa wa Mtwara, Amina Rajabu, akiwa na mganga mkuu wa mkoa wa Lindi dokta Genchwele Makenge kujadiliana masuala mbalimbali juu ya elimu wanayopatiwa katika mafunzo ya kujengewa uwezo yanayotolewa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 kwa ufadhili wa shirika la USAID. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara na kushirikisha watendaji wa sekta ya afya kutoka mikoa Mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dar es Salaam na Pwani.
|
No comments:
Post a Comment