JUMA MOHAMED, MTWARA
Baadhi ya
maafisa habari wa halmashauri mbalimbali katika mikoa ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma wanakabilia na changamoto ya uhaba wa vitendea kazi kwa ajili ya kazi
zao za kihabari, hali ambayo inapunguza ufanisi katika kazi.
Wakizungumza
na Juma News katika
semina ya kuwajengea uwezo maafisa habari wa mikoa hiyo, juu ya namna ya
kuendesha tovuti za serikali kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za
Umma PS3, walisema kutokana changamoto hiyo wanalazimika kutumia simu kwa ajili
ya kurekodi matukio, pale wanapokosa kuwa na kamera.
“Tunajua ni changamoto kwa baadhi ya
Halmashauri kukosa vifaa, lakini tunaweza kutumia njia ya kujiongeza kwa
kutumia simu..simu za sasaivi zina mfumo wa Android, kwahiyo ukiwa na simu
yenye Android unauwezo wa kurekodi Vidio vizuri na kuihariri..” alisema Teresia
Malian, ambaye ni afisa habari halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Naye
mtaalamu wa TEHAMA kutoka wizara ya TAMISEMI Edgar Mdemu, alieleza umuhimu wa
Tovuti katika kuimarisha sekta za umma, kabla ya katibu tawala wa mkoa wa
Mtwara Alfred Luanda, kusisitiza maafisa habari kuzingatia uzalendo katika kuchapisha
habari zao kwenye tovuti hizo.
“Kwa kupitia
hii ‘website framework’ basi naamini kwamba taarifa nyingi sana za halmashauri na
mikoa zitakuwa kwenye ‘website’ kwa ajili ya wananchi kuweza kupata taarifa
mbalimbali..” alisema Mdemu.
Semina hiyo
inayojumuisha maafisa habari na maafisa TEHAMA wa halmashauri na mikoa ya
Mtwara, Lindi na Ruvuma inatarajiwa kuhitimishwa Machi 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment