Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea na waandishi wa habari baada ya kukagua shughuli za uchongaji wa madawati zinazoendelea katika karakana ya halmashauri ya wilaya ya Mtwara. |
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Zacharia Nachoa, akiongea na waandishi wa habari katika karakana na uchongaji madawati ya halmashauri yake. |
Fatma Ally. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
SERIKALI
mkoani hapa imewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupunguza tozo
katika mbao zinazosafirishwa kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kutengezea
madawati kwa matumizi ya wananfunzi wa shule za msingi na sekondari.
Akizungumza baada
ya kutembelea karakana ya kutengenezea madawati iliyopo katika manispaa ya
Mtwara Mikindani, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, alisema jitihada
mbalimbali zinafanyika kwa ajili ya kutafuta fedha za kutatua tatizo hilo
lakini pesa nyingi zinatumika katika kilipia tozo hizo.
“Kinachooneka
wenzetu wa Maliasili bado hawajalitambua vizuri hili jambo la madawati,
kwasababu kunakuwa na vikwazo vingi tunavyovipata kutoka kwao hata pale sheria
zinapofuatwa unakuta bado tunakumbana na vikwazo..lakini kwasababu wote ni
serikali sisi tumeshaanza taratibu za kufanya mazungumzo nao ili waweze
kutupunguzia tozo zisizokuwa na msingi hasa kwenye hizi mbao za madawati..”
alisema.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatma Ally, akiwa amekaa katika dawati kwa ajili ya kujiridhisha juu ya ubora na kujua kama linakidhi kwa matumizi ya wanafunzi wa shule za msingi. |
Aidha,
alisema kasi ya utatuzi wa changamoto hiyo imekuwa kubwa kwa halmashauri zote
tatu za wilaya yake na kutoa matumaini kuwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu tatizo
hilo litakamilika kwa asilimia 100.
Alisema kwa
upande wa wilaya ipo mikakati ya aina tatu tofauti ambayo imejiwekea, miongoni
mwake ikiwa ni kuhakikisha kila halmasahuri inabadilisha matumizi ya fedha za
miradi mbalimbali na mapato yake ya ndani, na kuelekeza fedha hizo katika shughuli
za uchongaji wa madawati.
“Lakini pia
tumekuwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao tumewashirikisha ambao
tumewaomba misada na wanaendelea kuchangia, wapo ambao wameshangia na wapo
ambao tumewaomba na wameahidi watachangia..lakini sehemu ya tatu ni mfuko wa
mkuu wa wilaya ambao tumeanzisha kampeni inaitwa Haba na haba, hii moja kwa
moja inahusisha jamii na wadau ambao wapo mkoa wa Mtwara..” alisema.
Mafundi wanaochonga madawati ya halmashauri ya wilaya ya Mtwara. |
Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Zacharia Nachoa, alizitaka jamii kuunga mkono
jitihada hizo zinazofanywa na viongozi wao za kutatua changamoto hiyo huku
akiwapongeza wananchi wa tarafa ya Ziwani ambao kupitia kata zao wamehamasika
kwa kiasi kikubwa kuchangia kwa hiyari utatuzi wa tatizo hilo.
Salumu Juma,
mkazi wa manispaa ya Mtwara, aliipongeza serikali ya wilaya na mkoa kwa ujumla
kwa jitihada za dhati wanazozifanya katika kuhakikisha wanawaokoa wanafunzi
kutoka katika adha ya kukaa chini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Zacharia Nachoa, akiongea na waandishi wa habari katika karakana na uchongaji madawati ya halmashauri yake. |
“Mazingira
ya elimu yalikuwa ni magumu, kwahiyo sasa hivi kama serikali inachukua upeo huu
wa kuweza kunufaisha elimu kwa wakazi wake wa Mtwara sisi tunashukuru na
tunaomba waendelee hivihivi wawe na moyo wakibinadamu watusaidie hivi kama
wanavyotusaidia, na wanavyovifanya vinaonekana na hii ndio serikali ambayo sisi
tulikuwa tunaihitaji..” alisema.
Mafundi wakiwa kazini |
No comments:
Post a Comment