Salum Telela wa Yanga (Kushoto) akimtoka mchezaji wa Coastal katika moja ya michezo ya Ligi kuu ya Tanzania Bara. (PICHA: MTANDAO) |
![]() |
Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya magoli yao yalifungwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya African Sports (PICHA: shaffihdauda.co.tz)
Na Juma Mohamed.
TIMU ya soka
ya Coastal Union ya Tanga leo imefanikiwa kusitisha rekodi ya mabingwa watetezi
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc ambao walikuwa hawajawahi
kufungwa tangu kuanza kwa msimu huu, baada ya kuichakaza magoli 2-0 katika
mchezo uliopigwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mchezo huo
ulioamuliwa na Endrew Shamba kutoka mkoani Pwani ulikuwa wakushambuliana kwa
pande zote huku wenyeji wakionekana kudhibiti vilivyo sehemu ya kiungo cha
Yanga na kufanikiwa kupunguza mashambulizi ya mfululizo langoni mwao.
Wauwaji wa
Coastal leo walikuwa ni Miraji Adam aliyeandika goli la kwanza kipindi cha
kwanza kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja na kumshinda mlinda lango
wa Yanga Deogratius Munish ‘Dida’ huku Juma Mahadhi akipachika goli la pili
kipindi cha mchezo kwa shuti kali lililowababatiza walinzi na kumchanganya
Dida.
Kupoteza kwa
Yanga katika mchezo huo ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa
klabu hiyo Dkt. Damas Tiboroha kubwaga manyanga, inakuwa ni mara ya kwanza toka
kuanza kwa msimu huu kwani kabla ya hapo hawakuwahi kupoteza mchezo wowote
zaidi ya sare 3 ambazo walizipata.
Coastal sasa
wanafikisha alama 13 baada ya kucheza mara 16 wakisogea mpaka nafasi ya 11 na
kuipiku Ndanda ambayo ina alama 12 ikiwa inasubiri kushuka dimbani kesho na
Mgambo Shooting ya Tanga, huku Yanga ikiendelea kusalia kileleni mwa ligi kwa
alama zao 39 sawa na Azam ambao wanawazidi wastani wa magoli ya kufungwa na
kufunga baada ya kushuka dimbani mara 16 huku Wanalambalamba wakiwa wameshuka
dimbani mara 15.
Katika
mchezo mwingine uliopigwa leo uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba wameendeleza
wimbi la ushindi baada ya kuisambaratisha African Sports magoli 4-0 ikiwa ni
mwendelezo wa matokeo mazuri anayoyapata kocha mpya Jackson Mayanja aliyeshika
nafasi ya Dylan Kerry.
Mabao ya
Simba leo yamefungwa na Mganda, Hamis Kiiza aliyefunga mawili katika dakika za
14 na 42, Hassan Kessy dk 31 na Haji Ugando aliyepachika la mwisho katika dk 75
na kuifanya Simba kufikisha alama 36 ikisalia katika nafasi ya Tatu baada ya
kucheza mara 16.
|
No comments:
Post a Comment