Mwandishi wa habari wa Mtukwao Media-Gregory Milanzi, akitekeleza majukumu yake. |
Na Juama
Mohamed.
WANANCHI
wametakiwa kuwa makini katika ufuatiliaji wa vipindi mbalimbali vya Redio na
Televisheni na kuwasilisha maoni yao katika Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) iwapo wanabaini ukiukwaji wa maadili kutoka kwa
watangazaji.
Akizungumza jana
mkoani hapa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Margaret Munyagi, alisema
wasikilizaji wana haki ya kulalamika katika kamati hiyo iwapo wanabaini kuwepo
kwa dosari za kimaadili kwa watangazaji kiasi cha kusababisha uchochezi au
uvunjifu wa amani.
Waandishi wa habari |
“Watumiaji
wa huduma hii wana haki ndani ya mujibu na kanuni ambazo zinatawala utangazaji,
kwahiyo mtumie haki mliyonayo kama wasikilizaji..mna kofia mbili mnatoa huduma
lakini pia taarifa iwafikie watumiaji waliopo ili watumie fursa hiyo kuweza
kuleta malalamiki..unaposikia kipindi na maudhui na hujaridhika nayo unaona
kabisa ni kinyume na utamaduni wan chi hii na ukiona kwamba kuna uchochezi, una
haki kabisa kama msikilizaji kuileta kwenye kamati kwa ajili ya kuweza
kuishughulikia..” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui-TCRA, Margaret Munyagi. |
Alisema,
mamlaka kupitia kamati hiyo inaimiza matumizi ya Lugha sanifu na kwamba kwakua
Kiswahili ndio Lugha ya Taifa hapa nchini, vyombo vya habari kupitia vipindi
vyao vina wajibu wa kuhakikisha kwamba lugha hiyo inakuzwa na kutambulika zaidi
Kimataifa.
Alisema,
chombo cha habari cha Taifa kama ilivyo kwa Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) kina wajibu mkubwa wa kukuza lugha kutokana na dhamana iliyonayo na
kukemea watangazaji wanaotumia lugha za mkato na ambazo hazipaswi kusikika
katika vyombo vya habari.
Mjumbe wa kamati ya maudhui ya TCRA-Abdul Ngarawa |
“Tunajua
kabisa kama Uingereza kupitia chombo chao cha Taifa kile BBC ndio kiini cha
kuhakikisha kwamba lugha yao inakua na kutumika vizuri, kwahiyo tunategemea na
sisi kupitia vyombo hivi vitatumika kabisa kukuza lugha yetu ya Kiswahili
sanifu kabisa..lakini pia tunatambua kuwa Kiingereza kinatumika katika nchi
hii, basi Kiingereza kinachotumika kiwe sanifu mjitahidi sana..” aliongeza.
Aidha,
alitaja majuku ya kamati hiyo kuwa ni pamoja na kumshauri waziri wa habari juu
ya sera inayohusu mambo ya utangazaji hapa nchini, kusimamia utekelezaji wa
kanuni za utangazaji, maudhui/vitu vinavyotangazwa kupitia Redio na Televisheni
pamoja na kuchambua malalamiko ya wasikilizaji.
Afisa sheria mwandamizi wa TCRA-Hassan Mwanga, akifafanua jambo |
Naye, afisa
sheria mwandamizi wa mamlaka hiyi, Hassan Mwanga, alitoa rai kwa waandishi na
watangazaji wa Redio na Tv kufuata maadili ili kuhepuka kuchukuliwa hatua za kimaadili
na mamlaka, kwani wapo ambao wameonesha kukiuka na mara kadhaa wameitwa katika
kamati.
No comments:
Post a Comment