Friday, July 10, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA

 


 Manchester United wataongeza bidii kumfuatilia mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 25, baada ya kukubali kumuuza Robin van Persie kwenda Fernabahce (Daily Star), Van Persie amesema anahisi "kusalitiwa" na anaondoka Old Trafford baada ya miaka mitatu (Sun), kipa wa Stoke Asmir Begovic, 28, anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 8 kwenda Chelsea, huku kiungo Marco van Ginkel, 22, akitoka Chelsea kwenda Stoke kama sehemu ya mkataba huo (Daily Telegraph), Sevilla, West Ham na Orlando wanamtaka mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 ambaye kwa sasa ana jeraha la bega (Daily Mail), Newcastle United lazima walipe pauni milioni 15 kwa QPR kama wanataka kumsajili Charlie Austin, 26 (Evening Chronicle), Tottenham wanataka pauni milioni 15 kwa winga Andros Townsend ambaye anasakwa na Atson Villa na Sunderland (Daily Mail), Liverpool wanajiandaa kumtangaza kiungo Jordan Henderson, 25, kuwa nahodha wao mpya baada ya kuondoka kwa Steven Gerrard aliyekwenda Los Angeles Galaxy (Liverpool Echo), Manchester City wamesafiri kwenda Australia kwa ziara ya kabla ya kuanza kwa msimu, wakiwa na wachezaji vijana 17. Wachezaji wanane tu wa kikosi cha kwanza wamesafiri- Willy Caballero, Richard Wright, Vincent Kompany, Gael Clichy, Samir Nasri, Fernando, Jesus Navas na Yaya Toure ndio wamesafiri (Manchester Evening News), Jose Mourinho anakaribia kumsajili kiungo kutoka Chile Charles Aranguiz anayechezea Internacional kwa pauni miliono 16, huku John Obi Mikel akitarajiwa kuondoka (Metro). 

SOURCE: SALIM KIKEKE

No comments: