RYAN GIGGS ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MUDA WOTE WA PREMIER LEAGUE - HUKU BABU FERGIE AKIWA KOCHA BORA
Ryan Giggs ametangazwa
kuwa mchezaji bora wa muda wote katika historia ya Premier league - huku Sir
Alex Ferguson akichukua tuzo kocha bora wa Barclays Premier league
history.
Fergie na Giggs wamechukua tuzo hizo wakati ligi hiyo ikisherehekea miaka 20 ya mfumo wa premier league.
Fergie na Giggs wamechukua tuzo hizo wakati ligi hiyo ikisherehekea miaka 20 ya mfumo wa premier league.
Giggs ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi na kushinda makombe mengi ya premier league chini ya uongozi wa Sir Alex Ferguson.
Mchezaji wa zamani wa United na kocha msaidizi wa England Gary Neville alisema: "Ryan Giggs ndio mchezaji kiingereza atakayebakia kuwa aliyefanikiwa zaidi kwa muda wote na sioni mchezaji mwingine wa kuja kuzivunja rekodi zake na kumpita.
"Amevunja na kuzipita kila rekodi katika suala la kuchukua makombe ndani ndani ya mipaka ya nchi hii. Mchezaji ambaye anafurahisha kumuona akicheza kila wiki."
Wakati huo huo kikosi cha Arsenal kilichomaliza ligi bila kufungwa kimetajwa kama kikosi bora - Arsenal walimaliza ligi bila kufungwa mwaka 2003/04.
Alan Shearer alitajwa kama mfungali bora wa muda wote akiwa na magoli 260 - huku David James akitajwa kama golikipa mwenye clean sheets nyingi(173)
Neville, Giggs, na Shearer pia walitajwa kwenye kikosi bora kabisa cha premier league history.
MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA YAPANGWA.
Orange
CAF Champions League draw:
Group
A
Sunshine
(Nigeria)
Esperance
(Tunisia)
AS Chlef
(Algeria)
ESS
(Tunisia)
Group
B
Ahly
(Egypt)
TP Mazembe (RD
Congo)
Berekum Chealsea (Ghana)
Berekum Chealsea (Ghana)
Zamalek
(Egypt)
Orange
CAF Confederation Cup 2nd 1/8 finals
MAS (Morocco)
v Léopards de Dolisie (Congo)
El Hilal
(Sudan) v CO Bamako (Mali)
AFAD (CIV) v
WAC (Morocco)
Djoliba (Mali)
v Club Africain (Tunisia)
Dynamos
(Zimbabwe) v Interclube (Angola)
Stade Malien
(Mali) v COD Meknès (Morocco)
Coton Sport
(Cameroon) v El Ahly Shandy (Sudan)
TAKWIMU: CRISTIANO RONALDO VS IONEL MESSI - NANI ZAIDI MWEZI WA 5 - NA MSIMU MZIMA.
TAKWIMU ZA MWEZI WA TANO |
280 | MINUTES PLAYED | 279 |
7 | GOALS | 3 |
4 | PENALTIES | 1 |
0 | ASSISTS | 1 |
15 / 7 (46.7%) | TOTAL SHOTS / ON GOAL | 25 / 11 (44%) |
127 / 104 (81.9%) | PASSES / COMPLETED | 90 / 61 (67.8%) |
7.8 | GOAL.COM AVERAGE RATING |
7.0 |
46 | 2011-12 LA LIGA GOALS | 50 |
65 (56) | 2011-12 COMPETITIVE GOALS (APPEARANCES) | 57 (52) |
http://i1.goal.com/files/images/stats/goal/team-logos/1/451_48x48.jpg
TAKWIMU ZOTE ZA MSIMU WA
2011-12 LA LIGA
|
3406 | MINUTES PLAYED | 3483 |
50 (37) | GOALS (GAMES) | 46 (38) |
10 | PENALTIES | 12 |
15 | ASSISTS | 12 |
201 / 98 (48.7%) | TOTAL SHOTS / ON GOAL | 260 / 103 (39.6%) |
2439 / 1995 (81.8%) | PASSES / COMPLETED | 1529 / 1175 (76.8%) |
7.46 | GOAL.COM AVERAGE RATING |
7.24 |
72 (59) | 2011-12 COMPETITIVE GOALS (GAMES) | 60 (55) |
http://i1.goal.com/files/images/stats/goal/team-logos/1/451_48x48.jpg
ANTONIO VALENCIA ATAWALA TUZO ZOTE ZA KLABU YA MANCHESTER UNITED
NANI KAWAFUNIKA WENZIE HAPA???/ |
KWA MARA YA KWANZA NDANI YA MIAKA 84 - RONALDO NA MESSI WAFANIKIWA KUWA WACHEZAJI WALIOFUNGA MAGOLI ZAIDI YA 120 KWENYE MSIMU MMOJA.
EUROPE'S GREATEST
GOAL-SCORING SEASONS | |||
PLAYER
|
GOALS
|
SEASON | |
L. Messi (Barcelona)
|
72
|
2011-12
| |
G. Muller (Bayern)
|
67
|
1972-73 | |
F. Deak
(Szentlorinci)
|
66
|
1945-46 | |
G. Zsengeller (Ujpest)
|
65
|
1938-39 | |
D. Dean (Everton)
|
63
|
1927-28 | |
J. McGrory (Celtic)
|
62
|
1927-28 | |
C. Ronaldo (Madrid)
|
60
|
2011-12 | |
R. Resmja (Tirana)
|
59
|
1950-51 | |
J. McGrory (Celtic)
|
59
|
1926-27 | |
F. Roberts
(Glentoran)
|
59
|
1930-31 | |
F. Deak
(Ferencvarosi)
|
59
|
1948-49 |
TAARIFA KUTOKA TFF
ASPIRE KUANZA
KUSAKA VIPAJI MEI 21
Mchakato wa
kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa
kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka
huu.
Vituo
vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na
tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout)
kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani
Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
Vingine ni
Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam
(Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam
(Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).
Mpango wa
Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16
duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika,
Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata.
Watoto
watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa
nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi,
Kenya.
Watakaofuzu
kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of
excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza
vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.
TWIGA STARS
KUJIPIMA KWA BANYANA BANYANA
Timu ya Taifa
ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya
Afrika Kusini (Banyana Banyana) itakayofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Twiga Stars
inayojiandaa kwa mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa
Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia imeingia tena kambini jana (Mei 14 mwaka huu)
kujiwinda kwa mechi hiyo itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis
Ababa.
Banyana
Banyana pia iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya Fainali za Nane za
AWC ambapo katika raundi hii ya pili imepangiwa Zambia na itaanzia mechi hiyo
ugenini jijini Lusaka.
Mei 12 mwaka
huu Twiga Stars ilicheza mechi ya kimataifa ya kujipima nguvu dhidi ya Zimbabwe
(Mighty Warriors) iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kambi ya timu iko
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu mkoani Pwani.
Naye Kocha
Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa katika kuimarisha kikosi chake
kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Banyana Banyana amemwita tena kikosi
mshambuliaji mkongwe Esther Chabruma.
Wakati huo
huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Rwanda
kuchezesha mechi hiyo ya AWC kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia.
Waamuzi hao
ni Angelique Tuyishime atakayepuliza filimbi wakati waamuzi wasaidizi ni
Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga. Kamishna wa mchezo
huo wa kwanza ni Catherine Adipo kutoka Uganda.
Mechi ya
marudiano itachezwa Dar es Salaam wiki mbili baadaye ambapo mshindi atapata
tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazofanyika Novemba mwaka huu
nchini Equatorial Guinea.
WATUNISIA
KUICHEZESHA STARS ABIDJAN
Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Tunisia na Misri
kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi kati ya Taifa
Stars na Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
Mwamuzi
atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote
kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri.
Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa
waamuzi (referee assessor) ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa
pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment