RASMI LIVERPOOL YAMTUPIA VIRAGO DALGLISH
Published: 56 minutes ago
KENNY DALGLISH amefukuzwa na Liverpool baada ya miezi 16 ya kufanya kazi.
Mkataba
wa Mcotland huyo umevunjwa wakati yeye akiwa Marekani.
Licha
ya kuiongoza klabu hiyo, kutwaa Komeb la Ligi maarufu kama Carling Cup na
kucheza fainali ya Kombe la FA, ambako ilifungwa kwa utata na Chelsea, lakini
kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu kumemponza.
Ikiwa
imemaliza katika nafasi ya naneLigi Kuu- hiyo ni kinyume cha matarajio ya klabu
hiyo, kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Liverpool
imemaliza msimu ikiwa na pointi 52 —ambazo ni chache zaidi kihistoria katika
ushiriki wao kwenye Ligti, wakizidiwa kete na wapinzani wao wa Merseyside,
Everton.
Wakali
hao wa Anfield pia walishinda mechi chache mno kihistoria msimu huu, 14, tangu
msimu wa 1953-54 na wamfunga mabao machache zaidi (47) tangu msimu wa
1991-92.
Wamiliki
wa timu pia hawakufurahishwa na jinsi alivyokuwa akimchukulia Luis Suarez
.
Dalglish
alitua Liverpool akirithi mikoba ya kocha wa sasa wa England, Roy Hodgson
Januari mwaka jana.
YANGA WAMPONZA KIIZA, ATEMWA THE CRANES, OKWI NDANI
Kocha wa The Cranes, Bobby Williamson leo ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Angola na Senegal kuwania Fainali za Kombe la Dunai mwaka 2014, huku akimoiga chini mchezaji huyo matata.
The Cranes itakwenda Luanda, Angola Juni 3, mwaka huu kucheza na wenyeji kabla ya kumenyana na Senegal mjini Kampala, Juni 9. Liberia ni timu nyingine kwemnye kundi lao.
Kikosi kamili cha Cranes ni; Makipas: Denis Onyango (Sundowns, SA), Posnet Omwony (Leopards, SA), Abel Dhaira (IBV, Iceland), Hamza Muwonge (Bunnamwaya),
Mabeki: Simeon Masaba (URA), Denis Guma (Victoria University), Isaac Isinde (St George, Ethiopia), Henry Kalungi (Richmond Kickers, USA), Godfrey Walusimbi (Bunnamwaya), Hassan Wasswa (Kayseri, Turkey), Joseph Ochaya (KCC), Andy Mwesigwa (Ordabasy, Kazakhstan), Habib Kavuma (APR, Rwanda), Edward Ssali (Bunnamwaya), Joseph Owino (Azam, TZ)
Viungo: Mike Sserumaga (St George, Ethiopia), Tonny Mawejje (IBV, Iceland), Musa Mudde (Sofapaka, Kenya), Patrick Ochan (TP Mazembe, DRC), Martin Mutumba (AIK, Sweden), Dan Wagaluka(APR, Rwanda), Moses Oloya (Sai Go, Vietnam), Sula Matovu (St George, Ethiopia), Mike Mutyaba (El Merreikh, Sudan)
Washambuliaji: Brian Umony (Becamex Binh Doung, Vietnam), Emma Okwi (Simba, TZ), Caesar Okhuti (Bunnamwaya), Robert Ssentongo (URA), Geoffrey Massa (Yenicami, N. Cyprus), Fabian Kizito (Leonidas, Netherlands)
No comments:
Post a Comment