MANCINI AMUOMBA RADHI FERGUSON
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini
amemuomba radhi kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa kitendo ch
mshambuliaji wake, Carlos Tevez kubeba bango la R.I.P. Fergie katika
kusherehekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England jana.
WENGER, CEO ARSENAL WAMUITA FARAGHA VAN PERSIE
MSHAMBULIAJI
Robin van Persie wa Arsenal, kesho anatarajiwa kuwa na kikao kizito na kocha wa
klabu yake, Arsene Wenger na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis
kuzungumzia mustakabli wake kwa Washika Bunduki hao.
Majadiliano
hayo, yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Wenger, kuanzia saa 4:00 kwa saa za
Uingereza.
Uamujzi
wa mwisho utachukuliwa kabla ya kutajwa kwa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi
Alhamisi, kinachotarajiwa kushiriki Euro 2012 na Van Persie anatarajiwa kuwamo.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba
wake, amemaliza msimu na mabao 41 katika mechi 53 za klabu na nchi yake.
Akiwa
amefunga mabao 37 katika 48 za Arsenal na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa
mabao yake 30 kwenye mechi 38, Van Persie sasa amegeuka lulu na klabu nyingi
kubwa Ulaya zinataka kumsajili
MAN CITY YATANGAZA OFA RASMI KWA VAN PERSIE
Tetesi J'nne Magazeti ya Ulaya
MAN CITY HAITANII KWA VAN PERSIE, INAMTAKA KWELI...
MABINGWA wapya wa Ligi Kuu
ya England, Manchester City wako kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Nahodha wa
Arsenal, Robin van Persie kwa dau la pauni Milioni 25, wakimuahidi mshahara wa
pauni 250,000 kwa wiki.
BAHATI
iliyoje kwa Arsenal, mchezaji wao mpya, Lukas Podolski amesema kwamba atakuwa
akicheza washambuliaji watatu katika nafasi moja katika kikosi cha washika
Bunduki wa London msimu ujao.
KLABU
ya Manchester United imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia
Dortmund, Robert Lewandowski, baada ya mazungumzo yake na klabu yake juu ya
mkataba mpya kufa. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland, mwenye umri wa miaka
23, amefunga mabao 30 msimu huu.
KIUNGO
wa Lille, Eden Hazard amesema kwamba atajiunga na klabu ya Manchester msimu huu.
Hata hivyo, Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 21 hakusema itakuwa ipi kati ya
City au United.
KLABU
za Chelsea na Liverpool zinaelekea kumkosa kiungo wa Sao Paolo ya Brazil, Lucas
Moura, kutokana na Inter Milan kuonekana wameingia kwa gia kubwa zaidi katika
vita ya kuwania saini ya kinda huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka
19.
KLABU
ya West Brom inabangua bongo kama imsajili moja kwa moja, kipa Ben Foster
anayewadakia kwa mkopo au la. Mchezaji huyo Bora wa Mwaka wa The Baggies,
anatarajiwa kurejea timu ya Daraja la Kwanza, Birmingham msimu huu.
DALGLISH OUT LIVERPOOL
KOCHA
wa Liverpool, Kenny Dalglish amekwenda Boston kupambana kupigania ajira yake,
kufuatia tetesi kwamba kocha wa Wigan, Roberto Martinez anaweza kuchukua nafasi
yake Anfield.
Martinez
nimtu anayetakiwa, na Aston Villa inaaminika kumuweka Mspanyola huyo na kocha wa
Norwich, Paul Lambert katika orodha ya makocha inaowataka kurithi mikoba ya Alex
McLeish iliyemfukuza.
MARADONA
GWIJI
wa Argentina, Diego Maradona amesema alifurahia taji la ubingwa wa Ligi Kuu
England, ambalo walilitwaa Manchester City, akisema; "Kwa moyo wangu wote". Bao
la ushindi la City dhidi ya QPR, lilifungwa mkwewe, Sergio Aguero aliyemuolea
binti yake.
HIZI NDIZO SERA ZA BIN ZUBEIRY, MIGOGORO HAIPEWI NAFASI
NIKIWA mwandishi wa muda
mrefu, niliyelelewa katika misingi na maadili ya kitaaluma, napenda kuwaambia
wasomaji wangu kwamba, sitoi kipaumbele kwa habari za migogoro kwenye blog
yangu.
Nasikitika, sitakuwa naandika
habari yoyote ya mgogoro- nikiamini kabisa wakati umefika Watanzania tunapaswa
kubadilika na kuachana na desturi hiyo, badala yake kufikiria namna ya kujiletea
maendeleo.
Lazima tukubali kukabiliana na
changamoto- kwa kufuata misingi ya sheria na katiba- badala ya kuweka mbele
vurugu na uvunjaji wa sheria.
Kwa
sababu hiyo, tunaanzia na huu mgogoro wa Yanga unaoendelea hivi sasa, BIN
ZUBEIRY haitaupa nafasi. Sera kubwa ya BIN ZUBEIRY ni kuandika habari za
maendeleo, kuelimisha na kuburudisha wasomaji wake.
Siwezi kuingilia uhuru wa
blogs nyingine- au magazeti hata Radio na Televisheni, lakini kwangu narejea
kwenye mafundisho na uzoefu nilioupitia chini ya magwiji wa taaluma ya Habari
nchini, nikiwa mfanyakazi wa kampuni ya Habari Corporation (sasa Neww Habari)
tangu 1998 hadi nilipoacha kazi Mei 1, mwaka huuu.
Nasema, BIN ZUBEIRY ni kwa
habari za maendeleo, na si migogoro. Asanteni. Mungu ibariki Tanzania, bariki
sekta yetu ya michezo, iwe na amani mafanikio. Amin.
YONDAN, NIZAR KHALFAN WATUA YANGA
Kelvin Yondan |
Nizar Khalfan |
kuichezea timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Gazeti la Habari Leo limeandika kwamba, habari za uhakika zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka ndani ya Yanga, zilidai kwamba Yondan amesaini mkataba wa miaka miwili.
“Tayari tumeishasajili wachezaji wawili ambao ni Nizar Khalfan mwaka mmoja na Yondan, bado wengine watatu wakiwemo wa kigeni,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza kwamba mlinda mlango namba moja Yaw Berko, naye ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na wameondoka jana na mshambuliaji Keneth Asamoah kwenda kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko.
Gazeti hili lilimtafuta Salum Rupia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga kuelezea suala la usajili wa Yondan lakini hakupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuita
bila majibu.
Aidha, alipotafutwa Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga, alisema kwamba hahusiki na mambo ya usajili, mambo yote ya usajili aulizwe Rupia.
“Nisingependa kuzungumzia mambo ya usajili, mambo ya usajili muulizeni Rupia ndiye anajua,” alisema Nchunga.
Hata hivyo Nchunga kwa sasa yuko kwenye shinikizo ambapo wanachama wa klabu hiyo wanamtaka ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kuiendesha klabu hiyo.
Yondani hakupatikana kuzungumzia, hilo kwa kuwa amesafiri na timu yake ya Simba Sudan na wanatarajiwa kurejea leo.
Kwa muda mrefu Yanga walikuwa wakimsaka Yondan bila mafanikio. Mchezaji huyo ameshawahi kuingia kwenye mgogoro wa mara kwa mara na mashabiki na viongozi wa Simba
wakidai kuwa ni mamluki wa watani wao hao wa jadi.
VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA
Published: 14th May 2012
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy amestaafu soka.
Van
Nistelrooy mwenye umri wa miaka 35, amekuwa katika wakati mgumu tangu amejiunga
na Malaga akitokea Hamburg msimu uliopita, akifunga mabao matano tu katika mechi
32.
Licha
ya ukame wake wa mabao, ameisaidia klabu hiyo ya Hispania kumaliza ndani ya
Top-Four ya La Liga kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao na kufuzu
kucheza Ligit ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu
hiyo.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Uholanzi, alisema: “Jana ilikuwa siku yangu ya mwisho katika
soka ya kulipwa. Nilitaka kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini ni wakati wa
kuondoka.
“Nimefikia
kwenye kiwango cha mwisho cha ubora na siwezi kucheza kwa kiwango kinachotakiwa.
Siwezi kuagwa vizuri zaidi ya hivi,"alisema.
Van
Nistelrooy alianzia soka nyumbani kwao na klabu ya Den Bosch kabla hajahamia
Heerenveen na PSV Eindhoven, ambako alijijengea jina.
Baada
ya kutwaa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu Uholanzi, Eredivisie Golden katika
misimu ya 1998/99 and 1999/2000, alichukuliwa kwa bei mbaya na vigogo wa Old
Trafford.
United
ilimsajili Van Nistelrooy bila ya kujali kama alikuwa majeruhi wakati huo,
akisumbuliwa na maumivu ya goti aliloumia mazoezini.
Van
Nistelrooy alilipa fadhila kwa kolcha huyo Mscotland, kwa kumfungia mabao 150
katika mechi 219 ndani ya misimu mitano ya kuitumikia Manchester na kuipa taji
msimu wa 2002/03.
Baadaye
aliuzwa Real Madrid mwaka 2006, ambako alifunga mabao 53 katika misimu miwili,
akiiwezesha Real kutwaa mataji mawili mfululizo ya La Liga.
Lakini
akaumia tena na akaukosa karibu msimu wote wa 2008/09 na kuzidiwa kete na akina
Raul, Gonzalo Higuain na Karim Benzema katika msimu uliofuata.
Alitimkia
Hamburg ya Ujerumani alikocheza miezi 18 kabla ya kurejea Hispania kuchezea
Malaga.
Van
Nistelrooy pia amefunga mabao 35 katika mechi 70 za timu ya taifa ya Uholanzi—
ikiwemo aliyofunga kwenye Euro 2004, Kombe la Dunia 2006 na Euro 2008 — na
mfungaji bora wa pili kihistoria katika Ligi ya Mabingwa, akiwa ametikisa mabao
54 katika mechi 81.
Mechi
yake ya mwisho ilikuwa kati ya timu yake, Malaga ambayo walishinda 1-0 dhidi ya
Sporting Gijon.
SCHOLES ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED
Last Updated: 15th May 2012
PAUL SCHOLES ataendelea kuichezea Manchester United msimu ujao.
Kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 37, amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuendelea
kukipiga Trafford.
Kocha
wa Old Trafford, Alex Ferguson amesema: “Imefanyika. Anabaki.”
Ferguson
alikuwa ana wasiwasi msimu uliopita ungekuwa wa mwisho kwa Scholes akiwa na jezi
ya United na atakuwa na wasiwasi iwapo, iwapo atateuliwa kwenye kikosi cha Roy
Hodgson kwa ajili ya Euro 2012, kwani amekwishapendekezwa.
Pamoja
na hayo, kocha wa United anashawishika kuamini kiungo huyo atakuwa na moto ule
ule msimu ujao katika kukibeba kikosi cha Mashetani Wekundu kwenye harakati za
kurejesha taji.
MAN CITY WAMWAGIKA MITAA YA MANCHESTER, LILIKUWA BONGE LA PATI LEO
Published: Today at 19:04
MAN CITY walisherehekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England waliotwaa jana kwa kutembea mitaani na basi lao kubwa la wazi jioni ya leo katika Jiji la Manchester.
Mashabiki
walimwagika mitaani kuwapongeza mashujaa wao huku wakipigiwa wimbo waThe
Beatles, Hey Jude.
Vijana
wa Roberto Mancini, walitwaa taji hilo kiaina yake wakipata mabao mawili dakjika
za majeruhi na kushinda 3-2 dhidi ya QPR katika siku ya mwisho ya msimu.
No comments:
Post a Comment