Sunday, November 22, 2015

Dangote awapongeza Watanzania kwa ukomavu wa Demokrasia..

Aliko simu
Rais wa makampuni ya Dangote Aliko Dangote
Na Philipo Lulale, Mtwara.
Wananchi wa Tanzania wamepongezwa kwa kubadilisha uongozi wa nchi kwa amani na utulivu kupitia utaratibu wa kidemokrasia,hali ambayo inaelezwa ni kigezo muhimu kwa nchi kueendelea kuvutia wawekezaji wengi wa nje kuwekeza hapa nchini.
Rais na mtendaji mkuu wa makampuni ya Dangote ya Nigeria alhaji Aliko Dangote alitoa pongezi hizo katika kijiji cha Msijute wilaya na mkoa wa Mtwara, alipokuwa anazunguumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwanda chake cha saruji kinachotarajiwa kuanza uzalishaji wakati wowote wiki ijayo.
Alisema ana imani kuwa raisi mpya wa Tanzania ataendeleza mahali alipoachia mtangulizi wake na kuipeleka nchi kutoka ilipo,kwenda hatua nyingine ya maendeleo.
Alisisitiza kuwa licha ya kuendelea kuombea nchi hii na uongozi mpya,pia wawekezaji kama yeye wanatakiwa kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha uwekezaji endelevu utakaosaidia kuivusha nchi kutoka mahali ilipo sasa hadi hatua nyingine.
Kwa mujibu wa bw. Dangote watanzania wategemee fursa za ajira za kutokana kupitia uwepo wa kiwanda hicho kikubwa kuliko vyote katika ukanda wa Afrika mashariki na kati,kitakapoanza uzalishaji kwani kusafirisha mzigo wa tani milioni 3 unahitaji angalau malori makubwa ya mizigo kati ya 600 hadi 700 ambapo 30% yatakuwa ni kwa ajili ya Tanzania.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Dangote bw. Sada Ladambeki alieleza kuridhishwa na hotuba ya raisi Dr John Magufuli aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa bunge na kwamba kile kinachoonekana katika nchi ya Tanzania inatia moyo sana kuwekeza katika nchi hii kutokana na uwepo wa hali ya amani na utulivu.
Alisema kile alichosisitiza riais ni utawala bora katika maeneo yote ambapo watu lazima wafanye vitu kwa njia sahhi ili wawekezaji kama wao waweze kujiamni wanapowekeza hapa nchini.
“Kama kichwa kikiwa kizuri mwili wote utakuwa mzuri,kama kichwa kimeoza basi mwili wote umeoza hiyo ni kanuni ya samaki” alisisitiza alhaji Sada.
“ukiwa na kiongozi mzuri anayefanya mambo kwa usahihi kila kitu kitakwenda vizuri,tunamwamini na tutafanya kila tunaloweza kufanya kuweza kumsaidia” alikazia.
ESTER
Ester Baruti-mkurugenzi mkazi wa Dangote company.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa kampuni ya Dangote nchini Tanzania Ester Baruti amewataka watanzania,wawekezaji  na watendaji serikalini kwa ujumla kushirikiana ili kumsaidia raisi wa Tanzania kutimiza azma ya kuwatumikia watanzania na kukuza uchumi

Alisema kwa mujibu wa hotuba ya mheshimiwa Magufuli wakati wa uzinduzi wa bunge la 11,inaonyesha nia yake ya kuhakikisha Tanzania inafikia mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Ninaomba sana tupendane watanzania,tuheshimiane,kuacha kudharauliana na kuthamini michango ya kila mtu katika nchi” alisisitiza.
Kwa mujibu wa Baruti nchi yetu ina wageni wengi wanaokuja kwa shughuli mbalimbali,miongoni mwao wakiwemo wanaoitakia mema nchi yetu na wengine wasioitakia mema nchi yetu.
Aliko

Alhaj Dangote akiongea na waandishi wa habari katika eneo kilipo kiwanda chake katika kijiji cha Msijute mara baada ya kukagua

Alhaji Aliko Dangote amewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 600 kujenga kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara kinachosadikiwa kuwa kikubwa katika ukanda wa Afrika mashariki na kati na kina uwezo wa kuzalisha tani milioni 3 kwa mwaka na kwa sasa kiko katika hatua za mwisho kuanza uzalishaji.
Kutokana na hali ya amani na utulivu mwekezaji huyo anatarajia kuwekeza katika maeneo mengine ya uwekezaji hapa nchini ikiwemo kilimo.

Ameshashuka

Aliko Dangote akiongozana na wenyeji wake kwenda kwenye chumba cha wageni mashuhuri kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara










No comments: