SHAABAN NDITI ATUA COASTAL UNION, TIMU YAENDA ZIARANI UTURUKI
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Bara
mwaka 1988, Coastal Union ya Tanga wanatarajiwa kufanya ziara ya kujiandaa na
msimu mpya nchini Uturuki, Julai mwaka huu, huku habari zaidi zikisema
wamemsajili kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Mussa Nditi (pichani
kushoto) aliyewahi kuwika Simba SC.
Msemaji wa Coastal Union,
maarufu kama Wagosi wa Kaya, Edward ‘Edo’ Kumwembe ameiambia BIN
ZUBEIRY jioni ya leo kwamba wapo kwenye mchakato wa ziara hiyo na
utakapokamilika watatoa ratiba kamili.
Ingawa Edo, ambaye pia ni
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa soka katika gazeti la Mwanaspoti, hakusema
ziara hiyo imefadhiliwa na nani, lakini habari ambazo BIN ZUBEIRY
imezipata kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Barabara ya 13, Tanga
zimesema ni mchezaji wao wa zamani, Kassa Mussa.
Kiungo huyo hodari wa zamani
wa Mkoa wa Tanga, aliyekuwemo kwenye kikosi kilichochukua ubingwa wa Bara 1988,
kwa sasa anaishi Uturuki ambako inaelezwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kimaisha.
Tayari Coastal imekwishaanza
mchakato wa kuunda kikosi ‘baab kubwa’ cha msimu ujao na habari zaidi zinasema
wako mbioni kumsajili kiungo wa zamani wa Simba, Mkenya Jerry Santo wakati
wachezaji wengine ambao viwango vyao vimeshuka kama Ben Mwalala, Mkenya pia na
Ramadhan Wasso, Mrundi, wamekwishaonyeshwa mlango wa kutokea.
Coastal inatarajiwa
kutengeneza ‘bonge la mshituko’ kwa wapenzi wa soka nchini katika usajili wao,
kutokana na harakati zao za chini chini za usajili wanazofanya, ikiwemo
kumsajili kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Mussa Nditi.
Wengine ambao tayari wamenasa
kwenye rada za Coastal ni mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Nsa Job
Mahenya ambaye msimu huu alichezea Villa Squad iliyoshuka daraja.
UKRAINE, CROATIA WATAJA VIKOSI VYA UBINGWA
Kocha wa Croatia, Slaven Bilić. |
KIKOSI
KAMILI CHA CROATIA:
MAKIPA: Stipe Pletikosa (FC Rostov), Ivan Kelava (GNK Dinamo Zagreb), Danijel Subašić (AS Monaco FC).
MAKIPA: Stipe Pletikosa (FC Rostov), Ivan Kelava (GNK Dinamo Zagreb), Danijel Subašić (AS Monaco FC).
MABEKI: Jurica
Buljat (Maccabi Haifa FC), Vedran Ćorluka (Tottenham Hotspur FC), Danijel
Pranjić (FC Bayern München), Gordon Schildenfeld (Eintracht Frankfurt), Josip
Šimunić (GNK Dinamo Zagreb), Darijo Srna (FC Shakhtar Donetsk), Ivan Strinić (FC
Dnipro Dnipropetrovsk), Domagoj Vida (GNK Dinamo Zagreb).
VIUNGO: Milan
Badelj (GNK Dinamo Zagreb), Tomislav Dujmović (FC Dinamo Moskva), Ivo Iličević
(Hamburger SV), Niko Kranjčar (Tottenham Hotspur FC), Luka Modrić (Tottenham
Hotspur FC), Ivan Perišić (Borussia Dortmund), Ivan Rakitić (Sevilla FC), Ognjen
Vukojević (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Eduardo
(FC Shakhtar Donetsk), Nikica Jelavić (Everton FC), Mario Mandžukić (VfL
Wolfsburg), Ivica Olić (VfL Wolfsburg).
Kocha wa Ukraine, Oleg Blokhin |
KIKOSI
KAMILI UKRAINE
MAKIPA: Oleksandr Goryainov (FC Metalist Kharkiv), Maxym Koval (FC Dynamo Kyiv), Andriy Pyatov (FC Shakhtar Donetsk).
MAKIPA: Oleksandr Goryainov (FC Metalist Kharkiv), Maxym Koval (FC Dynamo Kyiv), Andriy Pyatov (FC Shakhtar Donetsk).
MABEKI: Bohdan
Butko (FC Illychivets Mariupil), Olexandr Kucher (FC Shakhtar Donetsk), Taras
Mikhalik (FC Dynamo Kyiv), Yaroslav Rakitskiy (FC Shakhtar Donetsk), Yevhen
Selin (FC Vorskla Poltava), Yevhen Khacheridi (FC Dynamo Kyiv), Vyacheslav
Shevchuk (FC Shakhtar Donetsk).
VIUNGO: Olexandr
Aliyev (FC Dynamo Kyiv), Denys Garmash (FC Dynamo Kyiv), Oleh Gusev (FC Dynamo
Kyiv), Yevhen Konoplyanka (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Serhiy Nazarenko (SC
Tavriya Simferopol), Ruslan Rotan (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Anatoliy
Tymoshchuk (FC Bayern München), Andriy Yarmolenko (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Andriy
Voronin (FC Dinamo Moskva), Marko Dević (FC Metalist Kharkiv), Artem Milevskiy
(FC Dynamo Kyiv), Yevhen Seleznyov (FC Shakhtar Donetsk), Andriy Shevchenko (FC
Dynamo Kyiv)
MAAJABU YA MICHEZO, MESSI ALILIMWA KADI NYEKUNDU YA MOJA KWA MOJA 2005
Messi amewahi kupewa kadi nyekundu mwaka 2005 |
WAIJUA
ASILI YA MCHEZO WA DARTS?
Inaelezwa
kuwa mchezo huu ulianza katika nchi za Jumuiya ya Madola barani ulaya ambapo
wanajeshi walikuwa na utaratibu wa kulenga miti kwa kutumia vishale kama sehemu
ya mafunzo ya kulenga shabaha.
Kufuatia
mazoezi hayo ndipo watu wengine wakaanza kuiga na kuanzisha mchezo wa
Darts.
XX
HII NDIYO
PENATI YA KWANZA KABISA
Penati ya
kwanza kabisa kupigwa katika historia ya mchezo wa soka ilikuwa kwenye mechi
kati ya Wolverhampton Wanderers dhidi ya Accrington.
Mechi
hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Molineux siku ya Septemba 14 mwaka
1891.
Kwa
mujibu wa historia hiyo mchezaji wa Wolves Billy Heath ndiye aliyeweka historia
ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga penati mara baada ya kupewa mpira ili aweze
kupiga.
XXX
MPIRA WA MEZA WAWEKA REKODI YA
AJABU
Septemba 26 mwaka 2010 pale
mjini Guangzhou katika uwanja wa Guangzhou mchezo wa mpira wa meza uliweka
rekodi ya aina yake baada ya kuingiza watazamaji wengi zaidi kuliko
kawaida.
Mara zote tumekuwa
tukishuhudia mchezo wa soka, ngumi,tenis, kikapu ama netiboli ikiingiza
mashabiki wengi zaidi uwanjani ikilingamnishwa na michezo midogo kama
darts,skwashi, mpira wa meza pamoja na mingineyo.
Lakini hii ilikuwa ajabu
kwenye mchezo wa mpira wa meza ambapo kwenye uwanja wa Guangzhou nchini China
jumla ya watazamaji 1,197 waliingia kutazama mchezo huo.
Rekodi hiyo bado inaendelea
kutamba na imefanya mechi hiyo kuwa kubwa kuliko zote duniani katika michezo
yote iliyochezwa ya mpira wa meza.
XXX
MAAJABU YA MESSI KUONYESHWA
KADI NYEKUNDU
MESSI kama tunavyofahamu ni
kwamba mara nyingi amekuwa si mkorofi ndani ya dimba ikiwemo kupigana na
wachezaji wenzake ama kucheza rafu za hatari.
Hii imefanya wapenzi wengi wa
soka kuzua mjadala mkali wa mabishano ambapo wapo wanaosema kwamba MESSI amewahi
kupata kadi nyekundu huku wengine wakisema kuwa hana kadi nyekundu tangu aanze
soka lake.
Ukweli ni kwamba mchezaji
LIONEL MESSI amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu tena ya moja kwa
moja.
Kadi hiyo nyekundu aliipata
mwaka 2005 wakati akiwa anaichezea timu ya taifa ya Argentina ya vijana wenye
umri chini ya miaka 20.
Akiwa anaichezea timu hiyo
dhidi ya Hungary katika mechi ya kimataifa ya kirafiki, MESSI ambaye wakati huo
alikuwa na miaka 18, alionyeshwa kadi nyekundu.
MESSI alionyeshwa kadi hiyo
katika kipindi cha pili cha mchezo wakati akijaribu kumzuia kwa mkono beki wa
Hungary aliyemvuta jezi kwa nyuma wakati akielekea katika lango la
Hungary.
Katika tukio hilo MESSI ambaye
alikuwa kwenye kasi ya kuelekea langoni mwa timu pinzani ghafla alijikuta
akivutwa jezi na beki VILMOS VANEZAK na mara tu alipojaribu kupeleka mkono wake
kwa nyuma kwa bahati mbaya ukampiga shingoni mwa beki huyo na kumuumiza, kitu
ambacho kilipelekea mwamuzi kumpa kadi nyekundu.
Mechi hiyo ilimalizika kwa
timu ya vijana ya Argentina kupigwa bao 2-1.
XXXX
WAMJUA ALIYECHEZA MECHI NYINGI
ZAIDI ENGLAND?
Mchezaji huyo si mwingine bali
ni golikipa mstaafu wa kimataifa wa Uingereza PETER SHILTON ambaye amecheza
jumla ya mechi 1005 za ligi kuu ya Uingereza na kuweka rekodi ya
kipekee.
Mbali na rekodi hiyo PETER
SHILTON bado anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuichezea timu
ya taifa ya Unigereza mechi nyingi zaidi kushinda mwingine
yoyote.
Ni kwamba hadi sasa SHILTON
anatamba na rekodi ya kuichezea Uingereza jumla ya mechi 125 na kwa ujumla
alistaafu soka mnamo mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 47.
Full name Peter Leslie Shilton
Date of birth(1949-09-18) 18 September 1949 (age
62)
Place of birth Leicester, England
Playing position Goalkeeper
XXXXX
By ARONE
MPANDUKA(Radio Tumaini) kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mtandao wa
Intaneti.
MCHAKATO MISS WORLD WAANZA RASMI TANZANIA
Salha Israel, Miss Tanzania 2011 |
KAMPUNI ya Lino International
Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, imewataka warembo wanaotaka kushindana
katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya
Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika
kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.
Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim Lundenga ameiambia BIN ZUBEIRY jioni
hii kwamba sema kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili
ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika
mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng
Fitness Center Stadium, mjini Ordos, Inner Mongolia, China.
Lundenga alisema kuwa zoezi
hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na wakati huo, jumla ya
warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa
kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi
karibuni.
Alisema kuwa amefurahishwa na
kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi
ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la
Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian
Sarcos.
“Tunakaribia kufanya
mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo
wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia
katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa mpaka sasa jumla
ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32
pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano
hayo.
Fomu za kuomba kushiriki
zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa
mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.
ENGLAND YATAJA KIKOSI CHA MWISHO
Rooney kulia na Wellbeck kushoto |
JINA | KLABU |
MAKIPA: | |
1. Joe Hart | Manchester City |
13. Robert Green | West Ham |
23. Jack Butland | Birmingham City |
MABEKI: | |
2. Glen Johnson | Liverpool |
3. Ashley Cole | Chelsea |
5. Gary Cahill | Chelsea |
6. John Terry | Chelsea |
12. Leighton Baines | Everton |
14. Phil Jones | Manchester United |
15. Joleon Lescott | Manchester City |
18. Phil Jagielka |
Everton |
VIUNGO: | |
4. Steven Gerrard | Liverpool |
7. Theo Walcott | Arsenal |
8. Frank Lampard |
Chelsea |
11. Ashley Young | Manchester United |
16. James Milner | Manchester City |
17. Scott Parker | Tottenham |
19. Stewart Downing | Liverpool |
20. Alex Oxlade-Chamberlain | Arsenal |
WASHAMBULIAJI: | |
9. Andy Carroll | Liverpool |
10. Wayne Rooney | Manchester United |
21. Jermain Defoe | Tottenham |
22. Danny Welbeck | Manchester United |
No comments:
Post a Comment