UFARANSA YATAJA KIKOSI HATARI TUPU
Benzema, ataongoza safu ya ushambuliaji |
BLANC'S SQUAD FOR EURO 2012 |
MAKIPA | |||
Cedric Carrasso | Bordeaux | Steve Mandanda | Marseille |
Hugo Lloris | Lyon | ||
MABEKI | |||
Gael Clichy | Manchester City | Philippe Mexes | AC Milan |
Mathieu Debuchy | Lille | Adil Rami | Valencia |
Patrice Evra | Manchester United | Anthony Reveillere | Lyon |
Laurent Koscielny | Arsenal | ||
VIUNGO | |||
Hatem Ben Arfa | Newcastle | Florent Malouda | Chelsea |
Yohan Cabaye | Newcastle | Blaise Matuidi | PSG |
Alou Diarra | Marseille | Samir Nasri | Manchester City |
Yann M'Vila | Rennes | Franck Ribery | Bayern Munich |
Marvin Martin | Sochaux | Mathieu Valbuena | Marseille |
WASHAMBULIAJI | |||
Karim Benzema | Real Madrid | Jeremy Menez | PSG |
Olivier Giroud | Montpellier |
CHIPUKIZI 10 WAPITA MCHUJO ASPIRE
WACHEZAJI
10 wamepita katika mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya
miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko
chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
uliofanyika kuanzia Mei 21-26 mwaka huu.
Watoto zaidi ya 1,500
walishiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya mng’amua vipaji (scout)
Gisbert Xavier kutoka Hispania, na ulifanyika katika vituo vya Morogoro,
Bagamoyo mkoani Pwani, na Kawe, Makongo, Magomeni, Tabata, Kitunda, Tandika,
Ukonga na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa Dar es Salaam.
Kituo cha Morogoro
amechaguliwa Karim Hussein wa Shule ya Sekondari Nanenane, kituo cha Magomeni ni
Joseph Mushi wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere wakati kituo cha Tabata ni
Martin Tangazi.
Tandika ni Ismail Ngakonda
(Shule ya Sekondari Uwanja wa Ndege), Kitunda ni Nicholas Lauteri (Shule ya
Sekondari Ulongoni), Omari Mbwai (Shule ya Sekondari Msongola) na Hamad Omari
(Shule ya Sekondari Ulongoni).
Kituo cha Ukonga ni James
Msuva (Shule ya Sekondari Makongo) wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ni
Adolf Mtasigwa (Shule ya Sekondari Loyola) na Ally Hatibu (Shule ya Sekondari
Kurasini).
Mng’amuzi huyo wa vipaji
anatarajia kufanya mchujo wa mwingine kabla ya chipukizi hao kwenda Nairobi,
Kenya kwenye mchujo wa mwisho baada ya kambi ya ya siku nne kuanzia Juni 5-9
mwaka huu.
MAKOCHA COPA COCA COLA
KUSHIRIKI SEMINA YA FIFA
Makocha 35 wameteuliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushiriki semina ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa
Coca-Cola.
Semina hiyo itafanyika kwenye
ofisi za TFF jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi
kutoka FIFA, Ulric Mathiot. Makocha hao wanatakiwa kuripoti Juni 3 mwaka huu
kwenye ofisi za TFF.
Makocha hao na mikoa yao
kwenye mabano ni Englihard Livigha (Mtwara), Joseph Sehaba (Dodoma), Ramadhan
Ramadhan (Mjini Magharibi), Shaha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Salum Ali
Haji (Kusini Unguja), Mohamed Ali Khamis (Kaskazini Pemba), Mecky Maxime
(Morogoro) na George Simon (Kagera).
Haruni Dudu (Iringa), Maka
Mwalwisi (Mbeya), Amos Mewa (Rukwa), Athuman Kilundumya (Tabora), Charles Mayaya
(Shinyanga), Fulgence Novatus (Mwanza), James George (Mara), Amani Kongoro
(Kigoma), Mtoro Likere (Ilala), Evarist Katomondo (Kinondoni), Shawal Bilanga
(Temeke) na Rashid Chama (Arusha).
Wengine ni Francis Samatta
(Ruvuma), Issac Gamba (Kilimanjaro), Aloyce Mayombo (Pwani), Jomo Puccey
(Lindi), Justine Kanemela (Singida), Charles Msengi (Manyara), Mohamed Kampira
(Tanga), Alfred Itael (Arusha), Nicholas Achimpota (Dodoma), Leonard Jima
(Ruvuma), Leonard Malongo (Mwanza), Kesi Abdallah (Tanga), John Memba (Ilala) na
Zuhura Kapama (Kigoma).
Boniface Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment