Thursday, May 31, 2012

JOSE MOURINHO NA GUARDIOLA WAPEWA OFA YA MAMILIONI KUCHAMBUA SOKA LA EURO



Kituo cha Televison cha Televisa wamejaribu kuwaleta pamoja kocha Real Madrid Jose Mourinho na Pep Guardiola.

El Mundo Deportivo limesema Televisa wametoa ofa kwa Mourinho na kocha wa zamani a Barcelona Guardiola ya kiasi cha €1.5 million kwa kila mmoja ili kuweza kushea meza na kufanya uchambuzi wa soka kwenye michuano ya Euro 2012.

Ingawa, Mourinho bado hajatoa majibu kama amekubali au hapana, Guardiola yeye amekataa kabisa, akisistiza anataka kupumzika kabisa kutoka kwenye soka baada ya kuondoka Barca wiki hii.
Wakati wote wakiwa Barcelona Mourinho kama kocha na Guardiola kama mchezaji.
Watu maarufu maarufu ambao wameshawahi kufanya kazi na Televisa ni Luis Figo, Zinedine Zidane na Fernando Morientes.

MANCHESTER CITY, CHELSEA NA VILABU VINGINE EPL HATARINI KUKUMBWA NA ADHABU KALI KWA MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA

Vilabu vya English Premier League vimeonywa kushusha matumizi yao ya pesa, baada ya kutoka kwa ripoti ya matumizi ya fedha ya mwaka kuonyesha kwamba mishahara ya wachezaji ilikuwa imefikia level ya juu sana mpaka kuzidi ukuaji wa mapato ya vilabu hivyo.

Mishahara kwa ujumla imepanda kwa kiasi cha £201 kwenye msimu wa 2010-11, ikipanda kwa asilimia 14 mpaka kufikia takribani £1.6 billion - huku mapato yote ya vilabu yakipanda kwa asilimia 12 mpaka £2.27 billion - kutokana na taarifa za Deloitte.

Huku vilabu 20 vya juu vikitoa mishahara ili kuweza kuwavutia wachezaji wazuri katika harakati za kupata mafanikio, sasa hivi mishahara ya wachezaji inatumia asilimia 70 ya mapato yote yanayopatikana katika vilabu hivyo vya premier league.

Alan Switzer, mkurugenzi wa biashara ya michezo wa Deloitte, amewaonya wamiliki wa vilabu vinavyotumia fedha nyingi kwamba kutumia fedha vizuri kwenye mishahara ni muhimu, tena sasa ikizingatiwa sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA ikiwa inakaribia kuanza.

"Ikiwa uwiano wa mishahara na mapato ni asilimia 70 au zaidi, ni vigumu sana kuweza kufanya biashara ya faida," alisema.
"Kwa mtazamo wetu uwiano huo ni wa juu sana huku vilabu na league zikatakiwa kurudi kwenye asilimia 60 kwa mujibu wa sheria ya UEFA."

Upandaji wa mishahara kwenye baadhi ya vilabu vya ligi kumechangiwa na upandaji wa mapato ya kibiashara, klabu hizo zikiwemo Manchester United, Liverpool na Manchester City.

Figures hizi ni za msimu wa 2010-11 na utakuwa wa mwisho kabla ya sheria ya UEFA haijaanza rasmi kutumika na kutoa adhabu za kulipa faini au kufungiwa kushiriki kwenye mashindano ya shirikisho hilo kwa kosa la kutumia zaidi ya kile klabu inachotengeneza katika kutafuta mafanikio.

Switzer alisema mabingwa Manchester City na mabingwa wa ulaya Chelsea, zinazomilikiwa na Sheikh Mansour na Mrusi Roman Abramovich ndio wanakabiliwa na changamoto kubwa dhidi ya sheria ya FFP (Financia Fair Play).

"Chelsea na Manchester City ndio klabu ambazo zimeweka rekodi ya kupata hasara kubwa zaidi hivyo ndio zinazoweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kukumbwa na adhabu kali za FFP

No comments: