Na Juma
Mohamed.
KATIKA
kuendeleza utekelezaji wa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), inaendesha
mafunzo kwa walimu wa shule za sekondari katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa
ajili ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Hisabati, Baiolojia, Kiswahili na
Kiingereza.
Akizungumza
juzi na waandishi wa habari, afisa elimu kutoka idara ya usimamizi wa elimu
ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma, Hellen Msellem, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo
hayo, alisema mafunzo hayo yamewekwa mahususi kwa ajili ya kuinua kiwango cha
ufaulu katika masomo hayo ambayo katika miaka mitatu iliyopita wanafunzi
walionekana kuto fanya vizuri.
Alisema,
kutokana na mwaka huu kiwango cha ufaulu kuwa ni asilimia 80, imewekwa mikakati
itakayowawezesha walimu na wanafunzi kufikia malengo, ambapo miongoni mwake ni
pamoja na huo wa kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu ili na wao waende kuwafundisha
walimu wengine.
“Na kwa
mwaka huu kama sijakosea kiwango cha ufaulu kilichowekwa ni asilimia 80, sasa
ili kuweza kuifikia hiyo kuna malengo ambayo yamewekwa, moja wapo ni hili la
kuwawezesha walimu ili waweze kuangalia yale masomo ambayo watoto wanaonekana
wako chini katika ufaulu yaweze kuboreshwa katika ufundishwaji na hatimae kuna
wale wanafunzi ambao wana uwezo mdogo kwenye hayo masomo waweze kupewa masomo
yaziada..” alisema.
Kwa upande
wao, baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo, waliiomba serikali kuto ishia
katika masomo hayo manne pekee, isipokuwa mpango huo uendelee katika masomo
mengine kwani kwa kufanya ivyo itasaidia kwa kiasi kukubwa kuondoa tatizo la
kufeli kwa wanafunzi wengi hapa nchini.
“Jambo hili
ni zuri sana na naiomba serikali tusiishie tu katika masomo haya manne ya Baioliji,
Mathematics (Hisabati), Kiswahili na Kiingereza..watakapopata fursa kama hii na
wakawezeshwa kama tunavyowawezesha ambapo sasa tunauwezo wa kuwapambanua au
kuwatambua wale wazito kwa hizi hatua tulizofundishwa na hawa wawezeshaji, kwahiyo
itatuwezesha kubaini mapungufu ya motto, namna ya kumsaidia na mwisho wa yote
tutafuta ufaulu wa daraja sifuri muda mfupi ujao..” alisema mwalimu Khalidi,
kutoka shule ya sekondari ya Michiga, wilayani Nanyumbu.
No comments:
Post a Comment