Mashabiki wa Chelsea wakiwa na mbango ya kumpinga kocha wao |
Rafael Benitez, amesema kuwa aihama
klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu, na kutaja uamuzi wa kuumpa wadhifa wa
kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Akiongea baada ya kuiongoza Chelsea
kuishinda klabu ya Middlesbrough kwa magoli mawili kwa bila, katika mechi ya
raundi ya tano ya kuwania kombe la FA, kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile
aliwashutua mashabiki wa klabu hiyo.
Katika mahojiano na BBC, Benitez
amesema uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha kaimu kocha wa klabu hiyo, ilikuwa
kosa kwa sababu yeye ndiye kocha mkuu kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa
msaada wanaohitaji, na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.
'' Mashabiki sasa hawana sababu ya
kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Tamko hilo la kocha huyo wa zamani
wa Liverpool limejiri baada ya baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, kumdhihaki
baada ya mechi yao na Middlesborough.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52,
hajapata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo, tangu alipoteuliwa
kuchukua mahala pa Roberto Di Matteo mwezi Novemba mwaka uliopita.
Katika mechi nyingi zilizopita za
Chelsea, mashabiki wa klabu hiyo hawakuficha hisia zao za kutaka kocha huyo kuondoshwa.
No comments:
Post a Comment