Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu kucheza raundi ya tatu nay a mwisho kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.
Serengeti
Boys ilikuwa icheze raundi ya pili dhidi ya Misri; mchezo wa kwanza ukichezwa
Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na ule wa marudiano wiki mbili baadaye
jijini Cairo.
Katika raundi
ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka Denmark
ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo ilijitoa katika
michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi mwakani nchini
Morocco.
Serengeti
Boys sasa itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati ya
Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18 mwaka huu
jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini wiki mbili
baadaye.
Zimbabwe na
Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu,
Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano itafanyika kati
ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
Michuano ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia raundi ya
sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon
itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo Ruvu
Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na
Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew
Shamba.
Jumapili (Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).
No comments:
Post a Comment