Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.
Watazamaji
50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya
sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila
klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa
mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh.
70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Umeme sh.
750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi
sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh.
31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.
Wakati huo
huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja
wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000
imeingiza sh. 27,000.
Mgawo wa
mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja
sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh.
1,372.8 na DRFA sh. 915.2
No comments:
Post a Comment