YANGA ya Dar
es Salaam yenye maskani yake katika Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam leo
imefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kampuni ya bia (Tanzania Breweries
Limited – TBL) kilichopo Ilala jijini.
Akiongea
katika ziara hiyo afisa habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake imeamua
kufanya ziara yao katika kiwanda hicho ili kuweza kujionea mambo mbalimbali
ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji mbali mbali pamoja na bia
ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio wadhamini wakuu wa timu
hiyo.
Alisema kuwa
Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika mambo
mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi
pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo hivyo wamefurahishwa sana na jinsi
walivyopokelewa vizuri kiwandani hapo na aliwaomba waendelee na moyo huo huo wa
kuthamini timu yao.
“Tunawaomba
muendele na moyo huo huo kwani sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi
kutenganisha mafanyikio ya Yanga na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager na
kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha
ubora,” alisema Sendeu.
Awali,
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na
kitendo hiki cha timu hii ya Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea
kiwanda chao na kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani
hapo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager
inathamini mchango wa timu za Yanga kwa soka la Tanzania na ndio maana imekuwa
ikiidhamini timu hio huku akibainisha kuwa wataendela kudhamini timu ya Yanga
kwa muda mrefu.
Hivi sasa, thamani ya udhamini wa Kilimanjaro
Premium Lager kwa timu za Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani
1.5milioni(Shillingi Bilioni mbili) kwa mwaka kwa kila timu. Pesa hizi hutolewa
kwa ajili ya shuhuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wenye viwango vya
kimataifa, mabasi , vifaa vya michezo na
kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka na kuijengea uwezo team ya
Yanga.
“Tunafanya
hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni
dhahiri kuwa timu ya Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa
ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao. Ushirikiano wetu na timu ya
Yanga inatokana na ukweli kwamba Yanga ndio kati ya timu zenye wapenzi wengi
zaidi hapa nchini….timu ya Yanga pia ndio kati ya timu yenye historia yakipekee
hapa nchini na inachangia wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa Taifa Stars”
alisema.
Aliwasihi wananchi kwa ujumla na haswa washabik
wa Yanga kuendelea kuisapoti timu kufuatana na mafanyikio yake kwenye ligi na
mchango wake kwenye timu ya Taifa
na aliitakia Timu ya Yanga kila la
heri kwenye msimu wa 2012/2013.
Kavishe
alisema ndoa kati ya Kilimanjaro Premium Lager ni yenye mafanikio kwani ndani ya
Udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, timu hiyo imejipatia ubingwa katika
mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata mwaliko kutoka Ikulu ya Tanzania
na ile ya Rwanda baada ya kushinda ubingwa wa michuano ya Kagame kwa misimu
miwili mfululizo
SOURCE:BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment