Michuano ya
Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 28 mwaka huu) kwa
mechi za Super Weekend ambazo zitaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha
televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Mechi ya
kwanza ambayo itachezwa kesho itakuwa kati ya Azam na JKT Ruvu Stars. Mechi hiyo
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 1 kamili usiku kwa
viingilio vya sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A
kiingilio kitakuwa sh. 10,000.
Jumamosi
(Septemba 29 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Yanga
na African Lyon zitapambana Jumapili (Septemba 30 mwaka huu kwenye uwanja huo
huo kuanzia saa 11 kamili jioni.
Uwanja wa
Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1 mwaka huu kuanza
saa 10.30 jioni. Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1
kamili usiku.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea jana (Septemba 26 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi.
Zambi ambaye
anatarajiwa kuzikwa Jumapili (Septemba 30 mwaka huu) kabla ya kuwa kiongozi TOC,
kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho
wamepita kwake.
Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.
TFF inatoa
pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu
katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Zambi
mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment