
Akizungumza na Blog hii muda mfupi uliopita,mwenyekiti wa klabu hiyo Ismaili Aden Rage amesema kwamba, maamuzi yaliyotolewa na kamati ya sheria maadili na hadhi za wachezaji hayakuwa ya haki, na taarifa rasmi juu ya nini kitafanywa na klabu hiyo itatolewa kesho,mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Kamati ya sheria maadili na hadhi za wachezaji iliokutana juzi,iliamua pingamizi ambazo zilikuwa zimewekwa na Simba kuhusu wachezaji Mbuyu Twite na Kalvini Yondani kuichezea klabu ya Yanga ya Dar Es salaam.
No comments:
Post a Comment