BEKI Nemanja
Vidic ataanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wiki hii, kabla ya wachezaji
wenzake wa Manchester United kurejea kazini, wameandika Man Utd kwenye tovutui
yao. Beki huyo wa kati wa kimataifa wa Serbia, hajagusa mpira tangu goti katika
mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Basel, Desemba, mwaka
jana.
MASIKINI BERKO, AUMIA TENA
Yaw 'Poster' Berko |
KIPA namba moja wa mabingwa wa
soka wa Afrika Mashariki na Kati wa Young Africans Sports Club (YANGA), Yaw
Berko amepewa mapunziko ya siku tano kufuatia kuchanika katika paji la uso
wakati wa harakati za kuokoa mpira katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na www.youngafricans.co.tz ,Daktari
wa timu Juma Sufian amesema mchezaji huyo ameshonwa jumla ya nyuzi tano katika
paji lake la uso hivyo atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha siku tano
kuanzia kesho akiwa katika mapunziko.
Berko aliumia wakati akiwa
katika harakati za kuokoa krosi iliyochongwa na golikipa mwenzake na kuweza
kujigonga katika mlingoti wa goli na kusababisha kuchanika na kuweza kupata
matibabu ya haraka uwanjani hapo.
Mchezaji mwingine aliyeumia
katika mazoezi hayo siku ya leo ni Hamis Kiiza Diego ambaye aliumia katika eneo
la kidevu baada ya kombora lililoachiwa na mshambuliaji mpya Said Bahanuzi kutua
karibu na kidevu chake na kusababisha mchezaji huyo kugaagaa hadi alipopatiwa
matibabu na kuendelea na mazoezi hayo.
Mchezaji majeruhi ambaye
hakuweza kufanya mazoezi hayo ni Nurdine Bakari aliyeumia mwanzoni mwa wiki
hii.
YANGA NA EXPRESS YA UGANDA JUMAMOSI TAIFA
Yanga mazoezini ufukweni |
MABINGWA wa soka wa Afrika
Mashariki na Kati, Young Africans Sports Club,siku ya jumamosi wanatarajia
kujipima nguvu na Mabingwa wa Uganda timu ya Express pambano litakalopigwa
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya klabu
www.youngafricans.co.tz Mratibu wa pambano hilo
Frank Pangani amesema mipango ya mchezo huo tayari imekamilika ikiwemo Mabingwa
hao wa Uganda Express inayotarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam
wakitokea jijini mwanza ambapo mwisho wa wiki iliyopita ilicheza mchezo wa
kirafiki mjini Shinyanga.
Pangani amesema timu hiyo ya
Express kutoka Uganda ambayo hivi karibuni ilicheza na Simba katika uwanja wa
Kirumba inatarajiwa kuwa na msafara wa wachezaji na Viongozi jumla
26
Timu hiyo ya Express kutoka
nchini Uganda inarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi tayari
kwa mchezo huo wa Jumamosi ikiwa chini ya kiongozi wa msafara Mohamed Katerega
ambaye pia ni meneja wa timu hyo na msemaji wa timu ndugu Isack
Mumena.
Kwa upande wake Kocha msaidizi
Fred Felix Minziro amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi hivyo
pambano hilo pia litasaidia kikosi chake kujiweka sawa kabla ya michuano ya
Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu.
Minziro amesema anafurahishwa
na mazoezi yanayoendelea hivi sasa kutokana na bidii zinazofanywa na wachezaji
wake ikilinganishwa na Mwaka jana anaamini kuwa michuano ya Kagame na ligi Kuu
ya Vodacom itakapoanza timu yake itafanya vizuri katika michuano
hiyo.
Kocha huyo amesema tayari
ameona dalili za kila mchezaji kucheza kwa juhudi ili kuhakikisha kuwa kila
mchezaji anapata namba za kudumu katika kikosi chake.
MANJI AWEKEWA PINGAMIZI TFF ASIGOMBEE YANGA
Manji kulia, akiwa amechuchumamaa kujmsalimu Bi Rukia, mwanachama maarufu wa Yanga |
Na
Princess Asia
WAKATI
kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kuketi Julai
2 kwa ajili ya kupitia pingamizi zilizowasilishwa kwa wagombea uongozi wa klabu
ya Yanga, wagombea wawili Yusuf Manji na Stanley Yono Kevela wamewekewa
pingamizi.
Kwa
mujinu wa dinasimail.blogspot.com Klabu ya Yanga inatarajiwa
kufanya uchaguzi mdogo julai 15 jijini Dar es Salaam ili kuziba nafasi za baadhi
ya viongozi waliojiuzulu akiwemo mwenyekiti Lloyd
Nchunga.
Mjumbe wa kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti
wake Deogratius Lyatto, Salum Mbwezeleni alisema kwamba kamati yake itapitia
pingamizi hizo kwa kusikiliza wapingaji na waliopingwa na kisha kutoa
maamuzi.
Hata
hivyo, Mbwezeleni hakuweza kutoa ufafanuzi wa pingamizi wa wagombea hao Manji
(Uenyekiti) na Kevela (Makamu Mwenyekiti, Ujumbe) kwa madai kuwa bado hajapitia
maelezo yaliyowasilishwa na waliopinga.
“Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa kamati
itakutana Julai 2 na kuwasikiliza wahusika wote na kisha tutatoa maamuzi ili
majina yaweze kutangazwa na wagombea waanze kampeni zao,”alisema.
Kamati
ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji Mstaafu John Mkwawa wiki
iliyopita ilitawataja waliopitishwa katika ujumbe ni pamoja na Jumanne
Mwamenywa,Edgar Fongo, Beda Tindwa, Ramadhan Said,Omary A. Ndula, Shaban
Katwila,Ramadhan Y. Kampira,Lameck Nyambaya na Peter H. Haule.
Wengine
ni Justine S. Baruti,Abdalah A. Mbaraka, Kevela,Mosess K. Valentino,Aaron
Nyanda,George M. Manyama.Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo na Gaudiusus
Ishengoma.
Huku
wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ayoub Nyenze, Kevela na Clement A.
Sanga, wakati Jonh Paul Jambele, Manji, Edgar W. Chibula na Sarah Ramadhan
wameomba katika nafasi ya uenyekiti,”alisema.
Uchaguzi huo ambao umepangwa
kufanyika Julai 15 mwaka huu, umelenga kuziba nafasi ya Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya Utendaji ambao
walijiunzulu.
GARETH BALE AJITIA KITANZI MIAKA MINNE WHITE HART LANE
KLABU ya Tottenham imetangaza
kwamba Gareth
Bale amesaini mkataba mpya wa miaka minne, ambao utamuweka White Hart Lane
hadi 2016, wameandika Goal.com. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales,
kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na habari za kuhama klabu hiyo kwenda
Manchester United na Barcelona ambazo ziliripotiwa kumtaka nyota huyo mwenye
umri wa miaka 22.
SASA INAKUJA GREAT KILIMANJARO RUN GKR
Na Princess
Asia
BAADA ya mafanikio makubwa ya
kumleta mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount
Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout
Kilimanjaro Marathon 1991 imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run –
GKR”
GKR
zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 - 28 October 2012
zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili manjaro. GKR
itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na marathon siku
ya jumapili tarehe 28 October.
Akizungunzia uamuzi wa
kushirikisha mbio fupi katika GKR Rais wa klabu ya Mt. Kilimanbjaro Marathon
1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu yake inataka kuziendeleza pia mbio fupi na
michezo mingine ya uwanjani badala ya kuweka juhudi zote kwenye marathon
tu.“Watu wamekazania sana marathon na kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi
kuliletea taifa hili sfa kubwa sana” alisema Ngowi kwa
msisitizo.
Kuanzishwa kwa GKR kutaufanya
mji wa Moshi kuwa na mbio tatu za marathon kwa sasa na hii inaufanya mji huu
kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha kukuza na kuendeleza vipaji
vyao.
Tutamleta Haile Gabreselasie
aje kuzindua mbio hizi” alisema Ngowi ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo
marefu jijini Addis Ababa na gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya
Ethiopia. Ngoiwi aliweza pia kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia
(Ethiopia Airlines) jijini Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro
Marathon. Kwa sasa Ethiopia Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount
Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki kwenye
mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai duniani.
Aidha, ET wanalipia gharama za
kutangaza mbio hizi wakati wa New York Marathon, L.A Marathon na Boston
Marathon. Hii inaitangaza sana Tanzania kwani mbio hizi tatu zinawashirikisha
wakimbiaji wengi sana kutoka katika nchi nyingi duniani. Kwenye mbio hizi za
Marakani Mt. Kilimanjaro Marathon huweka banda la maonyesho linaloitangaza
Tanzania na vivutio vyake.
Pia
Mt. Kilimanjaro Marathom huchezesha nahati nasibu (raffle) kwenye mbio hizi tatu
za Marekani ili kuwapata washiriki maarufu kama Deidre Lorenz kuja kukimbia na
kuitangaza vyema Tanzania.
Aliendelea kusema kuwa nchi
hii ni yetu sote hivyo tuna jukumu la kuitangaza na kuiendeleza wote alisisitiza
Ngowi ambaye mwaka 2000 ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimpa
tuzo ya “Mwanateknolojia wa Karne ya 20” kwa juhudi zake za kuendeleza
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Ngowi anawaalika watu binafsi,
makampuni na taasisi kushirikiana naye kuendeleza Utalii wa michezo hapa
Tanzania ili kuipeleka nchi hii hatua moja mbele kwenye utandawazi. Kwa wale
wanaotaka kuwasiliana naye kuhusu ufadhili watumie anwani ya barua pepe
yangowio@yahoo.com au wapige simu namba 0754-360828.
No comments:
Post a Comment