Kikosi cha Simba msimu uliopita |
Na Prince
Akbar
MABINGWA wa soka Tanzania,
Simba SC wamethibitisha kushirikimichuano ya Kombe la Ujirani Mwema Tanzania,
iliyopangwa kuanza Jumapili wiki hii visiwani Zanzibar.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, Makamu Mwenyekiti
wa Simba, Geofrey Nyange, amesema maamuzi ya kushiriki katika mashindano hayo
yamefikiwa baada ya majadiliano baina ya uongozi, benchi la ufundi na Kamati ya
Ufundi ya Simba.
“Tumeamua kushiriki kwa sababu
tumeona haitakuwa vema kufanya hivyo wakati watu wa Zanzibar wametupa heshima
kubwa ya kutualika kwenye michuano hii. Kombe la Tanzania lina maana kubwa kwa
sasa kutokana na hali halisi ya kisiasa na kijamii iliyopo visiwani humo kwa
sasa,” alisema.
Makamu alisema zaidi ya
kushiriki michuano hiyo, Simba pia itatumia fursa hiyo kuweka kambi maalumu kwa
ajili ya kujiandaa na Kombe la Kagame lililopangwa kufanyika kuanzia Julai 14
mwaka huu.
Pia, alisema Simba itatumia
ziara hiyo kupeleka kombe la Ligi Kuu ya Vodacom kwa wana Simba wa Zanzibar
ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa ubingwa Vodacom na
pia.
“Tusisahau pia kwamba kabla ya
kucheza mechi yetu ya mwisho dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga ambayo
tulishinda kwa idadi ya mabao 5-0, Simba ilikwenda kuweka kambi Zanzibar,”
alisema Kaburu.
Simba itaanza michuano hiyo
siku ya Jumatatu ambapo itacheza na Mafunzo ya Zanzibar katika pambano
lililopangwa kufanyika usiku. Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Jumatatu jioni
lakini imesogezwa mbele hadi Jumatatu usiku.
Jumla ya timu nane zinashiriki
katika michuano hiyo ambapo Waekundu wa Msimbazi wapo katika kundi A lenye timu
za Simba, Azam, Mafunzo na timu ya soka ya taifa ya vijana ya Zanzibar wenye
umri wa chini ya miaka 23 (Karume Boys).
Wakati huo huo: Mabingwa hao
wa Tanzania, Simba SC, wanatarajiwa kucheza na mabingwa wa soka wa Uganda,
Express FC, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopangwa kuchezwa katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, maandalizi yote kwa ajili ya
pambano hilo yamekamilika na kwamba kikosi cha Simba kitaundwa na wachezaji
wapya na wa zamani.
Huu
utakuwa mchezo wa pili baina ya timu hizo, katika ziara hii ya Tae Wekundu wa
Kampala, baada ya awali kutoka sare ya 1-1 Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga.
SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA WARUNDI KAGAME, AZAM WAPEWA WAZENJI
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah. |
Na Prince
Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watafungua dimba na Atletico ya
Burundi katika mchezo wa Kundi C wa michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A,
wataanza na URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi wengine wa
Tanzania katika michuano hiyo, Azam FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar
katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Chamazi, Julai 15.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema katika
Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Ilala, Dar es Salaam kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) itashiriki kama timu mualikwa.
Aidha, habari za kusikitisha
ni kwamba, Musonye amesema Sudan, Ethiopia, Eritrea na Somalia hazitaleta
wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
Wakati Ethiopia ligi yao
inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi wao wapo kwenye michuano ya Afrika na
wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia wawakilishi wao Elman wamebadilisha
uongozi, hivyo bado hawajajipanga na Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji
wao kuzamia kila wanapokuja kwenye mashindano, wameondolewa.
“Wameondolewa, kwa sababu
mbili, kwanza nchi yao imeomba ipewe muda kulifanyia kazi sual hilo, na sisi pia
(CECAFA) tunalitafutia ufumbuzi,”alisema Musonye.
Lakini Musonye amekiri kitendo
cha kuyatoa mashindano hayo mwanzoni mwa mwaka hadi katikati ya mwaka
kumechangia baadhi ya timu kutoshiriki na amesema tayari amewasilisha pendekezo
kwenye Mkutano Mkuu, mashindano yarejee kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama
ilivyokuwa awali.
Kuhusu mechi ya ufunguzi ya
Simba kuchezwa Julai 16, ambayo itakuwa Jumatatu badala ya Jumapili, Musonye
alisema kwamba imetokana na kwamba Julai 15, Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali
za Copa Coca Cola, ambayo maandalizi yake yote yamekamilika.
Yanga ndiye bingwa mtetezi wa
mashindano, baada ya kuifunga Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
RATIBA
KAMILI KOMBE LA KAGAME
No comments:
Post a Comment