Friday, July 4, 2014

Mafua yazua taharuki kikosi cha Ujerumani

Bastian Schweinsteiger
 

 
                        
















Wachezaji saba wa Ujerumani wanaonyesha dalili za homa ya mafua, kabla ya mechi yao ya robofainali dhidi ya Ufaransa Ijumaa, kocha Joachim Loew alisema kwenye mahojiano kwenye redio ya Ujerumani bila kutaja wachezaji hao.
"Wachezaji saba wana dalili za homa ya mafua,” Loew alinukuliwa akiambia redio ya ARD. Alisema wengi wana “maumivu ya koo” lakini hakutaja majinao yao.
“Kutokana na hayp, ni mapema sana kuamua kuhusu watakaocheza,” Loew akaongeza.
Difenda Mat Hummels alikosa mechi ya Ujerumani ya 16 bora dhidi ya Algeria Jumatatu kutokana na homa. Alisema Jumatano kwamba amepona na akaweka mtandaoni picha yake akwia ameketi kwneye ufuo.
Kiungo wa kati wa akiba Christoph Kramer alikuwa akitatizwa na baridi mwilini Jumatano na alikuwa mchezaji pekee aliyekosa kufanya mazoezi, alisema kocha msaidizi Andreas Koepke, aliyeongeza kuwa wachezaji wengine wote wako sawa na tayari kuelekea Rio de Janeiro kwa mechi hiyo ya Ijumaa.
Loew amesema kwamba kusafiri Brazil kwenye maeneo tofauti ya hali ya hewa kucheza mechi zao nne kufikia sasa pamoja na kucheza mechi kwenye joto kali, mvua kubwa na baadaye baridi ya Porto Alegre – pamoja na mfumo wa kudhibiti hewa – kumewaathiri.
“Ninatumai kwamba wote wako sawa kwa sasa,” Loew alisema. Akaongeza: “Mambo si mabaya sana kwa sasa. Sitaki kuongeza chumvi.” Lakini Loew alisema hali ya Hummels imekuwa mbaya zaidi.
"Hali ya Mats Hummels ilibadilika na kuwa mbaya siku ya pili,” Loew akasema.
Loew amekosolewa sana Ujerumani kutokana na uamuzi wake wa kuweka nahodha Philipp Lahm safu ya kati badala ya ukabaji kulia, ambako ametamba kwa miaka mingi. Loew alilazimika kumuweka Lahm nafasi ya ukabaji kulia baadaye kwenye mechi dhidi ya Algeria kutokana na majeraha.

No comments: