Saturday, September 15, 2012

SIMBA WAANZA VYEMA LIGI KUU TAIFA LEO

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013 imeanza rasmi kutimua vumbi hii leo,ambapo timu zote 14 zimejitupa kwenye viwanja saba tofauti.

Mabingwa watetezi Simba wamewakaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,ambapo mchezo huo umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mabao ya Simba leo hii yamewekwa wavuni na Mshambuliaji mahiri Emanuel Okwi dakika ya 33 akiwatoka walinzi wa Lyon na kuachia shuti kali,lililokwenda moja kwa moja kimiani,wakati dakika chache baada ya kufungwa kwa bao hilo,African Lyon walipata Penalt,baada ya Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Baada ya kukoswa kwa Penalt hiyo,Simba walicheza counter atack,ambapo Cholo aligongeana na Mrisho Ngasa na kujipatia bao la pili,likifungwa na Ngasa.
Kipindi cha pili Simba waliendelea kutawala mchezo nakufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Daniel Akufo kwa mkwaju wa Penalt,baada ya Emanuel Okwi kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Mjini Morogoro, Polisi Dodoma wametoshana nguvu na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri baada ya kwenda suluhu ya bila kufungana, wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo imepanda daraja msimu huu imetandikwa bao 1-0 na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Tanzania Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu imetoshana nguvu na mabingwa wa kombe la Kagame Da Young Africans kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kwa kutofungana. JKT Ruvu na Ruvu Shooting zimepambana kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam,na Jkt Ruvu kupata ushindi wa 2-1, huku Azam ikiwazamisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba kwa kuwachapa bao 1-0.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwenyeji Toto Africans amepata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Oljoro JKT.

No comments: