Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula. |
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, akimsikiliza mzee kutoka kata ya Nanguruwe. |
Na Juma Mohamed, Masasi.
SERIKALI
imezitaka halmashauri nchini kutekeleza kwa vitendo nia ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ya kutaka kutatua changamoto
zinazowakabili wazee katika kupata huduma za afya, kwa kuwapatia kadi za kupata
matibabu bure.
Akizungumza
katika hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo, waziri wa afya, maendeleo ya
jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, alisema, Rais aliamua kwa
makusudi kuweka jina la wazee katika wizara ya afya kwa ajili ya kutambua kuwa
ni sehemu ya maendeleo ya jamii.
“Na wazee
kwakweli kero yao kubwa wao wala hawana shida ya kazi, lakini ni mbili uhakika
wa kipato na suala la matibabu..kwahiyo kama sisi sekta ya afya tukijitahidi
kuhakikisha wanapata matibabu, tunawaachia wenzetu wa wizara ya fedha wao wafanye
kazi ya kuwapa pensheni, na kazi imeshaanza kufanyika kwahiyo hili kwakweli ni
suala lakujipongeza..” alisema.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, akimsikiliza mzee kutoka kata ya Nanguruwe. |
Aidha,
waziri aliipongeza halmashauri ya mji Masasi kwa kuweza kuwalipia gharama za
matibabu kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wazee 780 ambao ni sawa na
asilimia 20 ya wazee 3,905 waliotambuliwa kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Alisema,
pamoja na kuonesha mfano nzuri kwa kuweza kulipia idadi hiyo lakini bado
wanatakiwa kuongeza juhudi ili angalau waweze kufikia asilimia 50 ya kuwalipia
wazee ambao wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kupata matibabu huku wengi
wao wakiwa na kipato duni.
“Kwakweli ni
changamoto kubwa kwasababu na Mhe. Rais ameamua kuwapa hadhi wazee..kwahiyo
ndio maana wizara hii angesema tu hatamki wazee, ukisema maendeleo ya jamii
unazungumzia wanawake, watoto na wazee lakini Mhe. Rais kwa ajili ya kuonesha
msisitizo wake akaamua wizara iwe na jina la wazee..” aliongeza.
No comments:
Post a Comment