Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
VYAMA vya
msingi mkoani hapa (AMCOS) vimetakiwa kuwa wawazi kwa kutoa mchanganuo wa
mapato na matumizi kwa wakulima wa zao la korosho baada ya kufanyika kwa minada
ili kuondoa malalamiko kwa baadhi ya wakulima hao ambao hawaridhishwi na
wanachokipata baada ya mauzo ya zao hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, alisema bado
hajaridhishwa na utendaji kazi kwa baadhi ya vyama hivyo na kuahidi kuchukua
hatua kwa vyama ambavyo vitashindwa kutekeleza agizo hilo kuanzia msimu ujao wa
korosho.
“Kwahiyo
Sitegemei chama chochote cha msingi kwanza kwenda kumlipa mkulima bila kumpa
taarifa ya mapato na matumizi, lakini kwasababu nalifuatilia kwa karibu na hua
Napata taarifa kutoka maeneo yote kupitia kwenye ofisi zetu rasmi na wakulima
wenyewe, bado nikiri kuna maeneo vyama vyetu va msingi vinaenda kinyume na
tulivyokubaliana..” alisema.
Aliwataka
wadau na viongozi wengine wa ngazi za chini kuhakikisha wanalinda masilahi ya
mkulima ambaye ndio chimbuko la kupanda kwa uchumi wa mkoa ambao kwa kiasi
kikubwa unachangiwa kwa kufanya vizuri kwa zao la korosho.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego. |
“Tukisimama
sisi viongozi wote na hasa wale maafisa wetu wa Ugani na ushirika mimi naamini
kabisa wakulima wetu hawatofanyiwa visivyo, lakini jamii hii wapo waliopotoka,
mimi nasema hatutacheka nao tutachukua hatua kali dhidi yao kwasababu tunataka
angalau mkulima wakati tunajipanga kuelekea kubangua korosho basi afaidike na
hiki kidogo ambacho kinapatikana..” alisema.
Alisema,
amewaagiza maafisa ugani, wakurugenzi na wakuu wa wilaya wote kupita katika
kila chama cha msingi kwa ajili ya kukagua taarifa na kujua kama wakulima
wameridhia na walichokipata na kama bado ifanyike jitihada za dhiada kuweza
kuwaridhisha.
Aidha,
alisema katika msimu huu uliomalizika, mkoa umeweza kufika na kuvuka lengo
kwasababu umeweza kukusanya jumla ya tani 100,006 huku lengo ambalo ulijiwekea
ilikuwa ni kukusanya tani 90,000.
“Na kwa
jinsi tunavyoijua korosho yetu tatizo kubwa ilikuwa ni bei kwa mwaka huu
mwenyezimungu amejaalia bei imeongezeka, lakini haijaja kwa kuongezeka tu
yenyewe imekuja kwa ajili ya kubanana lakini pamoja ni hilo ongezeko bado
sijaridhika, kama tutabangua korosho Mtwara hiyo bei tunayoiongelea sasa hivi
mkulima atapata mara dufu yake.” Aliongeza Dendego.
No comments:
Post a Comment