Gari likiwa barabarani katika barabara ya Kilambo |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WAKAZI wa
kijiji cha Kilambo, Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wamelalamikia ubovu wa
barabara kuanzia kijijini hapo kuelekea mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambayo
haikidhi kwa matumizi ya vyombo vya usafiri.
Wakizungumza
kijijini hapo kwa nyakati tofauti, walisema matengezo yanayofanyika katika
kuboresha miundombinu ya barabara hiyo sio sahihi kwasababu ya kufusi
kinachotumika kwa matengeno sio imara.
Walisema
serikali inapaswa kutilia mkazo ujenzi wa barabara hiyo kwasababu ndio
kiunganishi cha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji ambapo shughuli mbalimbali
zinazofanywa na wananchi wan chi hizo kwa kiasi kikubwa zinafanyika kwa kutumia
barabara hiyo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kilambo, halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakiwa barabarani katika barabara ya Kilambo inayoelekea mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. |
Kwa upande
wake, mwenyekiti wa serikali ya kikiji hichi, Mohamed Mkama, alikiri kuwepo kwa
changamoto hiyo na kudai kuwa jitihada za kuwasilisha taarifa za ubovu wa
barabara kwa uongozi wa halmashauri zinafanyika, lakini utekelezaji wake
unakuwa mgumu.
“Hii
barabara ni muhimu sana kwasababu inaunganisha nchi mbili pia watu ni wengi
kutoka nchi jirani na kuja huku na wanaotoka huku kwenda nchi jirani, kwahiyo
inaponyesha mvua kunakuwa na madimbwi na mashimo magari yanapita kwa shida,
wananchi vilevile wakiwa na baiskeli zao wanapata shida sana..kwahiyo tunaiomba
serikali hasa halmashauri iiangalie barabara hii ni muhimu zaidi.” Alisema.
No comments:
Post a Comment