Na Juma Mohamed, Mtwara.
TIMU ya soka
ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC Fc) imeendeleza ubabe
katika michezo yake baada yah ii leo kuwagalagaza wakusanya mapato, timu ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mtwara kwa kuwafunga magoli 3-0.
Katika mchezo
huo wa bonanza ambao ulianadaliwa na MTPC, timu zote zilionekana kuanza mchezo
kwa kasi huku zote zikicheza kwa tahadhari kubwa kuhepuka Kurusu mabao ya
mapema na kujikuta wakienda mapumziko wakiwa hawajafungana.
Kipindi cha
pili kilipoanza madiliko kadhaa yalifanyika kwa timu zote mbili ambayo hata
hivyo yalionekana kuwa na manufaa kwa MTPC ambao walifanikiwa kupata mabao
mawili ya haraka kupitia kwa kiungo wao Marick Mbuyu baada ya kupiga pasi ndefu
za kuonana kabla ya mfungaji kuwatoka walinzi wa TRA na kupachika mabao hayo ya
aina moja.
Baada ya
hapo TRA walijaribu kupanga mashambulizi kadhaa langoni mwa MTPC na kudhani
pengine wataweza kukomboa magoli hayo lakini baadae wakajikuta wanafungwa goli
la Tatu likifungwa na Hassan Mayamba baada ya kubabatizana na mlinzi wa TRA.
Mwamuzi
anapuliza filimbi ya mwisho kuashiria kumaliza mpambano huo, ni MTPC Fc ndio
ambao walioibuka mashujaa kwa ushindi huo mnono wa magoli 3-0 na kuendeleza
rekodi yao ya matokeo mazuri katika michezo wanayocheza uwanja wa Nangwanda,
huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwachapa mashabiki wa Ndanda Fc magoli 3-1
miezi kadhaa iliyopita.
Akizungumza
baada ya mchezo huo, kiongozi wa TRA, Isack Mgongolwa, alisema wamefurahi
kujumuika kwa pamoja na waandishi wa habari kwasababu wamepata fursa ya
kufahamiana na waandishi mbalimbali.
Alisema,
mechi za aina hiyo zinasaidia kuiweka miili katika hali nzuri kwasababu ni moja
ya mazoezi muhimu kwa ajili ya kujijenga kiafya huku akisisitiza kuwe na
mabonanza mengine kama hayo kwa ajili ya kujenga urafiki na wadau mbalimbali.
Akizungumza baada
mchezo huo, katibu wa MTPC na Nahodha wa timu hiyo, Bryson Mshana, aliwapongeza
wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kuonesha kiwango safi huku akiweka
wazi kuwa huo ndio utakuwa utaratibu wa taasisi hiyo ya wanahabari wa kuwa na
mabonanza kama hayo kila baada ya wiki mbili.
Alisema kitendo
hicho kitasaidia sana kujiweka karibu na taasisi mbalimbali na kujenga urafiki
baina ya wanahabari na taasisi jambo amablo ni muhimu katika kusaidia kulijenga
Taifa.
“Huu ni
utaratibu wetu na huu ni mwanzo tu lakini mipango yetu ambayo tumejiwekea ni
kuwa na mechi ambazo tutakuwa tukicheza na taasisi mbalimbali angalau mara
mbili kwa mwezi..hii itatusaidia sana kutujenga kiafya na kuweka ukaribu kati
yetu na wadau wetu..” alisema Mshana.
Naye,
mratibu wa bonanza hilo, Juma Mohamed, alliwataka waandishi wa habari kuona
umuhimu wa kushiriki kwa pamoja katika michezo kama hiyo kwasababu inasaidia
kuiaminisha jamii kuwa waandishi wa habari wapo karibu nao na wanajumuika
katika masuala mengine tofauti na taaluma yao.
“Mimi nitoe
wito tu kwa wanahabari wenzangu tuungane mkono katika haya masuala yakijamii
kwasababu tumepanga kuwa na haya mabonanza na shughuli nyingine za kijamii
ambazo tutafanya kwa utaratibu ambao tutajiwekea..nadhani itatusaidia sana
kwanza kuwa fiti kiafya lakini pia kujiweka karibu na jamii ambayo tunafanya
nayo kazi..” alisema na kuongeza:
“Nadhani
wote mnakumbuka tukio lililotokea katika mchezo wa Ndanda hapa siku chache
zilizopita na lilituhusu sisi kwasababu mwandishi mwenzetu alikamatwa na askari
wakati akitekeleza majukumu yake, sasa hii inaweza kutuokoa katika majanga kama
yale..” aliongeza.
No comments:
Post a Comment