Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi, Sospeter Nachunga (Aliyeshika mche wa Mti) akipanda mti. |
Na Juma Mohamed.
Halmashauri ya mji
Masasi kwa kushirikiana na wananchi inatarajia kupanda miti 395,170.00 ya aina
tofauti, katika maeneo mbalimbali wilayani humo kutoka kwa wazalishaji wa
Halmashauri hiyo, ambapo hadi hivi sasa imefikia asilimia 53.2 ya malengo hayo.
Hayo yamezungumzwa
na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Sospeter Nachunga, wakati akitoa taarifa
fupi ya siku ya upandaji Miti ambapo, alibainisha kuwa mkakati huo umepengwa
kutekelezwa ndani ya msimu huu wa 2015/2016.
Alisema, Tanzania ni
mojawapo ya nchi duniani zinazo kabiliwa na ongezeko la joto, hewa ukaa na
upungufu wa mvua, ambadiliko ambayo yamesababishwa na uharibifu wa kimazingira
kama vile ukataji wa miti kwa matumizi mbalimbali kulikopelekea vyanzo vya maji
kukauka katika maeneo mengi duniani, Tanzania, na hata katika eneo la
Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi, Sospeter Nachunga (Aliyeshika mche wa Mti) akipanda mti. |
“Kutokana na hali
hii ambayo ni tishio kwa vizazi vijavyo nchi yetu imejiwekea utaratibu wa
kupanda miti kila mwaka ambapo kila Wilaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua
1,500,000.. ndugu wananchi zoezi
hili ni jukumu letu sote kuhakikisha tunapanda miti katika maeneo yetu.” Alisema.
Aidha Mkoa wa Mtwara
umeweka utaratibu wa maadhimisho ya upandaji miti kwa mzunguko katika wilaya
zake saba. Katika mzunguko huo Halmashauri ya mji Masasi itakuwa mwenyeji wa
maadhimisho haya kimkoa mwaka 2021/2022.
No comments:
Post a Comment