Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara wa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John P. Magufuli,uliofanyika jana katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara. |
Na Juma Mohamed
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema iwapo wananchi watamchagua kuwa Rais, elimu itatolewa bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.
Akizungumza jana mjini hapa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa, Magufuli alisema ahadi hiyo itatekelezwa na itakuwa ni haki ya kila mwananchi na kwamba hakutakuwa na ubaguzi kwa kuangalia vyama vya kisiasa, dini wala kabila.
Alisema anafahamu machungu waliyonayo wananchi hasa wanavyowekeza nguvu zao kwenye kilimo ili kuhakikisha wanapata nguvu za kuwasomesha watoto wao, na kwamba njia pekee ya kupoza machungu hayo ni kuondoa gharama za kulipa karo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
“Tumepanga kuanzia mwaka kesho, wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne hakuna kulipa karo..nasema hakuna kulipa aa..karoooo, hakuna kulipaaa..karooo, ilo ndugu zangu ninaliweza wala musiwe na wasiwasi, wewe CCM hakuna kulipaaa..karooo, uwe Chadema hakuna kulipaaa..karooo, uwe UKAWA hakuna kulipaaa..karooo..” alisema huku akiitikiwa na umati wa watu waliojitokeza uwanjani hapo.
Elimu ya Juu
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John P. Magufuli, akiwahutubia wananchi wa Mtwara waliofurika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara |
Alisema, chombo kinachoshughulika na mikopo ambacho ni Bodi ya Mikopo, inatakiwa kuchukuwa tahadhari juu ya tabia hiyo ambayo inawakatisha tama wanafunzi wenye nia ya kufikia malengo yao.
Pia, alitoa ovyo kwa wanafunzi wenye tabia ya kuchukuwa mikopo na kuamua kutelekeza masomo kwa kufanya shughuli zingine, kwamba atahakikisha anawatafuta mpaka warudishe fedha zote walizochukua.
Maendeleo kwa wananchi
Aidha, alisema kuanzia mwakani kutakuwa na fedha za mikopo kiasi cha sh. Milioni 50 zitakazotolewa kwa akina mama na vijana kuanzia ngazi za mitaa, vijiji na kata, ambapo lengo likiwa ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi wote bila kuangalia itikadi ya vyama, kabila au dini zao.
Aliseema watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli ambayo hayahusiani na itikadi za vyama, na kwamba hakuna mtu aliyezaliwa na chama kwani vyama vya siasa vilikuja baadaye na mtu kuamua kushabikia chama anachokitaka lakini kwenye swala la maendeleo bado linakuwa ni la watu wote.
“Matatizo ni mengi, na kwa siku hizi imekuwa ni kawaida mtu ukienda hospitalini kumuona dakitari, utaandikiwa dawa na kuambiwa nenda ukanunue kwenye duka fulani..nasema serikali ya Magufuli haya hapana..ukienda hospitalini uwe CCM uwe CHADEMA uwe nani lazima madawa yote yapatikane hapo hapo..hizi fedha zilizokuwa zinapoteapotea tutaziwekeza ziende kwenye hospitali zikanunue madawa.” Alisema.
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John P. Magufuli, akimkabidhi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020, mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini, Hasnain Murji, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara |
Aliongeza kuwa, atahakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati, kila kata kunakuwa na kituo cha afya, kila wilaya iwe na hospitali ya wilaya na kila mkoa kuwe na hospitali ya rufaa kama ambavyo inafanyika katika mkoa wa Mtwara.
Ulinzi na usalama
Alisema atakuwa rafiki mkubwa wa majeshi yote nchini kwa kuyasimamia ili yafanye kazi vizuri na kuacha kuwa waoga pindi wanapopambana na majambazi kwa kuhofia wakiwapiga risasi watashitakiwa.
“Ukimpiga risasi jambazi aliye na silaha hakuna kushitakiwa..kwasababu saa nyingine tunawaogopesha polisi na wanajeshi wetu, mbona majambzi hawajaenda kituo cha jeshi la wananchi, mbona hawajavamia Ukonga na FFU..wanaogopa chamoto kipo kule..” alisema.
No comments:
Post a Comment