Wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Katani Ahmad, wakiwa wamebeba mfano wa jeneza wakiashiria kukizika Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu |
Mgombea ubunge jimbo la Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Katani Ahmad (mwenye flana la mistari) akiwasili katika viwanja vya shule ya msingi Mnyoma alikofanya mkutano wa kuzindua kampeni jana. |
Mgombea ubunge jimbo la Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Katani Ahmad (mwenye flana la mistari) akiwasili katika viwanja vya shule ya msingi Mnyoma alikofanya mkutano wa kuzindua kampeni jana. |
Na Juma
Mohamed.
JESHI la
Polisi wilayani Tandahimba mkoani hapa limetakiwa kuonyesha ushirikiano kwa
vyama vya upinzani wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya ubunge na
udiwani katika uchaguzi mkuu ili kuhepusha shari baina yao na wananchi.
Rai hiyo
ilitolewa juzi na mgombea ubunge wa jimbo la Tandahimba kupitia Chama cha
Wananchi (CUF), Katani Ahmad, wakati akizindua kampeni katika viwanja vya shule
ya msingi Mnyoma, kata ya Mdimba, ambapo alisema katika zoezi la kuchukua na
kurudisha fomu aliomba kibali cha kufanya maandamano ya amani na jeshi hilo
liliunga mkono na hakukuwa na shari yoyote.
Alisema,
kutokana na zoezi hilo kwenda vizuri, amekuwa na imani kubwa na jeshi hilo na
kwamba wanatakiwa kuendelea na msimamo huo huku akiwasihi kukataa iwapo
watapewa amri na viongozi wa juu za kuvuruga amani zitakazopelekea
kuwatofautisha na wananchi.
Bodaboda za wafuasi wa mgombea ubunge jimbo la Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Katani Ahmad, katika mkutano wa kuzindua kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Mnyoma, kata ya Mdimba. |
“Wapiga kura
watakapopiga kura na kura za Katani zikatosha, wanaojifanya nchi yakwao
wakasema nyie ndio mtumike, waambieni sisi hatutaki shari na wananchi hao..na
nimekuwa nikisema mara nyingi kwamba tatizo la raia na askari polisi limekuwa
likisababishwa na viongozi ambao hawana demokrasia ya kweli..wala sio tatizo
lao polisi hawa, wale wakubwa wakiona kiazi chao kinataka kuingia mchanga..na
ndio maana sisi katika katiba pendekezwa tulisema hatuhitaji kuona mkuu wa
wilaya akiwa kada wa Chama Cha Mapinduzi kwasababu ndio mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya..”alisema.
Na kuongeza
“ili polisi wakirusha bomu ni lazima mawasiliano baina ya watu hawa yawepo..OCD
(Kamanda wa Polisi wa Wilaya) na mamlaka yake hawezi kupiga bomu bila
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kusema sasa piga..” aliongeza.
Alisema
anaimani kuwa watawazidi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kura zaidi ya 20,000
jambo ambalo litawafanya washindwe na kukwamisha mipango na jitihada zozote
wanazozifanya katika kuhakikisha wanapata ushindi.
Aidha,
alitaja kipaombele chake iwapo wananchi wa Tandahimba watamchagua kuwa mbunge
kuwa ni kuboresha masilahi ya wakulima wa zao la korosho kwa kuhakikisha bei
inakuwa nzuri na yenye manufaa kwao, na kufanya kilimo cha muhogo kuwa kilimo
mbadala wilayani humo baadala ya korosho.
“na hili la
kilimo mbadala tayari nimeshalifanyia utafiti..mwaka jana nilikwenda nchini
China kwa ajili ya kujua Wachina wanahitaji kitu gani, bahati nzuri, hata
Muhogo ambao hatutii dawa Wachina wanahitaji..hawakuishia hapo, tukaingia
makubaliano kuona namna gani tunafanya kilimo cha Muhogo kuwa kilimo cha
biashara ndani ya mkoa wa Mtwara..” alisema.
No comments:
Post a Comment